Mmetuonea – Asema Zuchu Kuhusu Kufungiwa kwa Video Yao

Mwanamuziki wa Tanzania Zuhura Othman maarufu kama Zuchu ambaye anafanya kazi chini ya kampuni ya WCB Wasafi inayomilikiwa na Diamond Platnumz, amejibu hatua ya mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania TCRA ya kufungia video ya wimbo wake na Diamond uitwao, “Mtasubiri”. Zuchu ambaye ni binti wa mwimbaji maarufu wa Taarab Khadija Kopa amechapisha kipande cha video kilizua utata kwenye Instagram na kusema kwamba anahisi wameonewa.

Also Read
Juma Nature ateuliwa balozi wa Temeke

Zuchu alisema hatua kama hiyo inaashiria kifo cha tasnia ya muziki lakini akasema hisia zake hazifai kuchukuliwa kama ujeuri bali zipokelewe kwa heshima ya kutosha na utii. “Sisi ni vijana tunaotafuta rizki bila ya kuchoka lakini pengine Wazazi wetu ambao ni Baraza la Sanaa la Taifa, mmekua mstari wa mbele kutuvunja nguvu mbele ya jamii bila kujali hisia muda vipaji na uwekezaji unaofanyika.” aliandika Zuchu.

Also Read
Size 8 Reborn Azindua Albamu ya Kwanza

Msanii huyo alikumbuka jinsi yeye na wasanii wengine wa WCB walikosa kujumuishwa kwenye mgao wa mirabaha Wakati kitwakwimu wanaonekana kufanya vizuri kuliko wengine. Anataka kujua shidha iliyoko kutoka kwa BASATA na COSOTA shirika ambalo husimamia hakimiliki kwa niaba ya wasanii na hivyo kukusanya mirabaha kwa niaba yao.

Kuhusu Tuzo za Muziki, Zuchu haelewi ni kwa nini wanashtumiwa kwa kutoshiriki na kulingana naye ni wazi kwamba mashirika yote ya kusimamia sanaa yanapinga kampuni ya WCB.

Also Read
Sir Balo Achumbia Mpenzi Wake

Kwa mashabiki, Zuchu ametoa ahadi ya kuendelea na kazi huku akiomba msamaha kwa wasimamizi wa wasanii kwenye kampuni ya WCB. Hajafafanua iwapo watahariri video hiyo upya na kuondoa sehemu ambayo inasemekana kukera watu wa dini fulani.

  

Latest posts

Gravity Awataka Bebe Cool na Jose Chameleone Wastaafu

Marion Bosire

Kibao kipya cha Nonini kuzinduliwa siku ya kuzaliwa kwake

Tom Mathinji

Brenda Jons atangaza kuwa sasa ameokoka

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi