Mmishenari wa Marekani ahukumiwa miaka 15 gerezani kwa dhuluma za kimapenzi

Raia mmoja wa Marekani ambaye ni mmishenari amehukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani kwa kuwadhulumu kimapenzi wasichana wa umri mdogo katika makazi moja ya watoto aliyoanzisha katika kaunti ya Bomet.

Mahakama moja iliyoko Philadelphia, Pennsylvania, siku ya Alhamisi ilimhukumu Gregory Dow, aliye na umri wa miaka 61, kifungo hicho cha miaka 15 na miezi minane kwa kuwadhulumu kimapenzi watoto waliohitaji utunzi na ulinzi nchini kenya.

Dow alikiri kutekeleza maovu hayo mwaka jana akisema kuwa aliwadhulumu kati ya mwaka 2003 na 2017.

Wawili wa wasichana waliodhulumiwa kimapenzi walikuwa na umri wa miaka 11, mmoja alikuwa na umri wa miaka 12 na mwingine alikuwa na umri wa miaka 13.

Makao hayo ya watoto yalihudumu kati ya mwaka 2008 na mwaka 2017 wakati ambapo Dow aliondoka humu nchini.

Katika tangazo lililotolewea na kaimu mwanasheria mkuu wa Marekani Jennifer Arbittier Williams, Dow alitakiwa pia kulipa zaidi ya shilingi milioni 1.7 kwa kuwadhulumu kimapenzi wasichana wa umri mdogo katika makao ya watoto aliyoendesha na mke wake Boito katika kaunti ya Bomet.

Uchunguzi uliofanya na idara ya ujasusi wa Jinai hapa nchini DCI, kitengo cha kukabiliana na ulanguzi wa watu na ulinzi wa watoto pamoja na idara ya ujasusi ya Marekani FBI, uligundua kwamba Dow aliwadhulumu angalau wasichana wanne wenye umri mdogo kati ya mwezi obtober mwaka 2013 na mwezi Septemba mwaka 2017 kabla ya siri zake kufichuliwa.

Baadaye alitoroka kenya kuelekea jimbo la Lancaster nchini Marekani ambako alianzisha makao ya watoto huku akipata ufadhili kutoka kwa makanisa namashirika mengine ya kidini ya nchini Marekani.

  

Latest posts

Ruto: Mawakala wa kisiasa waliboronga uhusiano wangu na Rais Kenyatta

Tom Mathinji

COTU yazusha kuhusu nyongeza ya bei za mafuta nchini

Tom Mathinji

John Munyes na Charles keter kufika mbele ya Senate kuhusu ongezeko la bei ya mafuta

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi