Morris Kimuli aapishwa katika jopo la uteuzi la IEBC

Morris Kimuli ameapishwa kuwa mwanachama wa jopo la uteuzi litakalowajibika kujaza nafasi nne zilizoachwa wazi katika tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka humu nchini –(IEBC).

Kimuli aliapishwa na msajili mkuu wa idara ya mahakama Anne Amadi wakati wa sherehe fupi iliyoandaliwa katika mahakama ya juu.

Also Read
Mfungwa aliyehukumiwa kuhusiana na shambulizi la Chuo Kikuu cha Garissa ajitia kitanzi

Jopo hilo la uteuzi lenye wanachama saba sasa limekamilika.

Jaji mkuu Martha Koome, ambaye alihudhuria sherehe hizo za kuapishwa, alihimiza Jopo la uteuzi kuongozwa na katiba na pia maadili yake.

Mwenyekiti wa jopo hilo Elizabeth Muli aliahidi kutekeleza majukumu yake bila woga wala upendeleo.

Also Read
COVID-19: Kenya yanakili visa vipya 72 vya maambukizi

Kupitia arifa kwenye makala ya tarehe 26 mwezi Mei ya gazeti rasmi la serikali “Kenya Gazette”, Rais Uhuru Kenyatta alimteuwa Morris Kimuli kuchukua mahala pa Dorothy Jemator ambaye uteuzi wake ulibatilishwa.

Chama cha wana-sheria humu nchini (LSK) kilikuwa kimemteuwa Kimuli kuwa mwakilishi wake katika jopo la uteuzi la tume ya (IEBC).

Also Read
Visa 571 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Chama hicho kilikuwa kimepinga uteuzi wa Jemator kikisema anashikilia nyadhifa tatu za umma.

Wanachama wengine wa jopo hilo ni pamoja na Gideon Solonka, James Awori, Elizabeth Odindo Meyo, Joseph Mutie, na Suleiman Abdalla.

  

Latest posts

Prof. Magoha: Mtaala mpya wa elimu hautatupiliwa mbali

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Nelson Havi awasilisha rufaa ya kusimamisha mtaala wa CBC

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi