Mourinho apigwa teke Tottenham

Jose Mourinho amepigwa kalamu  kama meneja wa   Tottenham  Jumatatu siku 6 kabla ya timu hiyo kumenyana na  Manchester City kwenye fainali ya kombe la EFL Carabao.

Mourinho aliye na umri wa miaka  58,  amefurushwa Tottenham baada ya kuwa usukani kwa miezi 17 kutokana na msururu wa matokeo mabovu.

Also Read
Cheruiyot alenga ushindi wa tatu Diamond league

Taarifa hiyo imesema kuwa Mourinho na wasaidizi wake wote wamesimamishwa kazi  huku timu hiyo iking’ang’ana kumaliza miongoni mwa timu 4  bora  katika ligi kuu Uingereza ili kufuzu kwa ligi ya mabingwa  barani ulaya, ikiwa ya 7 ligini na pia ni maajuzi walipotimuliwa katika komb la  europa league katika raundi ya 16 bora  na Dinamo Zagreb.

Also Read
Kenya na Uganda kuzindua uhasama Cecafa U 17

Kocha wa Tottenham academy  Ryan Mason,  ameteuliwa kuwa meneja  wa muda hadi mwishoni mwa msimu huu , huku kocha wa

Also Read
Manchester United kucheza mechi 5 za ligi kuu Uingereza baina ya 9 na 23
Leipzig Julian Nagelsmann akipiwa upato kuwa mstari wa mbele kumrithi Mourinho sawia na meneja wa Leicester  Brendan Rodgers .
  

Latest posts

Malkia Strikers yafunga mechi za makundi kwa kuilaza Burundi seti 3-0 mashindano ya kuwania kombe la Afrika

Dismas Otuke

Waziri wa zamani wa michezo Hassan Wario afungwa miaka 6 gerezani na kulipa faini ya shilingi milioni 3 nukta 6

Dismas Otuke

Bingwa mara tatu wa dunia Justin Gatlin awasili tayari kushiriki Kip Keino Classic Jumamosi

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi