MP Shah yazindua mtambo wa kutengeneza hewa ya Oxygen

Vita dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 vimepigwa jeki kufuatia kuzinduliwa kwa mtambo wa kutengeneza hewa ya oxygeni katika hospitali ya MP Shah Jijini Nairobi.

Mtambo huo utakuwa na uwezo wa kutayarisha lita 500 za hewa ya oxygeni kwa dakika. Hospitali ya MP Shah kufikia sasa imetoa chanjo kwa watu 16,000.

Also Read
Mashemeji Ingwe na Kogalo kupimana nguvu fainali ya FKF CUP

Haya yanajiri huku shirika la utoaji huhuduma katika jiji la Nairobi likipania kuongeza idadi ya vituo vya afya vitakavyotoa chanjo ya COVID-19 kutoka 39 hadi 155.

Also Read
Idadi ya wasichana wanaochanjwa dhidi ya maambukizi ya HPV yapungua nchini

Akiongea wakati wa kuzinduliwa kwa ujenzi wa mtambo huo, mkurugenzi mkuu wa shirika la utoaji huhuduma katika jiji la Nairobi Meja jenerali Mohammed Badi alisema idadi ya vitanda katika hospitali ya Mbagathi imeongezwa hadi vitanda 220.

Also Read
Sabina Chege atishia kuongoza maandamano dhidi ya usimamizi wa jiji la Nairobi

Alisema kuna mipango ya kuzindua chumba cha wagonjwa mahututi chenye vitanda 26 katika hospitali ya Mama Lucy.

Wakati huo huo, nchi hii ilipokea msaada wa dosi 210,000 ya chanjo ya AstraZeneca kutoka Poland.

  

Latest posts

Aliyekuwa mtangazaji Mwanaisha Chidzuga ajitosa katika ulingo wa siasa

Tom Mathinji

#KisaChangu: Dr Mukhisa Kituyi kuwania urais ili kukamilisha safari ya ukombozi

John Madanji

Nyongeza ya bei za mafuta yapingwa Mahakamani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi