Mpango wa Imarisha afya ya Mama na Mtoto wazinduliwa upya Kakamega

Serikali ya kaunti ya Kakamega inashirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu hazina ya watoto UNICEF, kuzindua upya mpango wa Imarisha afya ya mama na Mtoto.

Mkuu wa shirika la UNICEF eneo la magharibi, Wangui Karanja amesema mpango huo unakusudiwa kuwasidia akina-mama na watoto kupata huduma bora za afya na lishe bora.

Also Read
UNICEF na USAID zatoa misaada ya barakoa kukabiliana na Covid-19

Serikali ya kaunti hiyo huwekeza shilingi millioni mia moja kila mwaka ambazo hutumiwa kumlipa kila mwanamke mja mzito na aliyejifungua kiinua mgongo na kuwatembelea mara sita.

Also Read
Oparanya aibuka Gavana mchapa kazi bora zaidi

Alikariri kwamba mpango huo huwapa motisha wanawake wajawazito kuhudhuria kliniki, kuhakikisha wanajifungua katika mazingira salama na pia kuhakikisha watoto wao wanachanjwa kwa wakati ufaao.

Vile vile wanawake wanaohitaji kupanga uzazi huweza kupokea huduma hiyo.

Also Read
Tuzo za Soya kuandaliwa Januari 19 kaunti ya Kakamega

Wangui alisema mpango huo hulenga siku elfu moja za kwanza za maisha ya mtoto ili kuhakikisha wanaishi katika hali nzuri ya afya.

Mpango huo umeunga mkono wanawake 65,000 kwa ushirikiano na serikali ya kaunti hiyo tangu mwaka 2014.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi