Mpango wa shirika la umoja wa mataifa kuhusu ustawi wa kiviwanda wazinduliwa

Rais  Uhuru Kenyatta amezindua mpango wa shirika la umoja wa mataifa kuhusu ustawi wa kiviwanda wa gharama ya dola bilioni 30 za Marekani ili kusaidia kusisimua sekta ya utengenezaji bidhaa hapa nchini.

Mpango huo kwa jina Programme for Country Partnership (PCP) Starter Pack, ni mpango wa kusisimua ustawi wa kiviwanda katika mataifa wanachama wa shirika hilo la UNIDO kwa kuhamasisha rasil mali za uwekezaji katika sekta za kiuchumi.

Mpango huo ambao pia unazinduliwa katika mataifa ya Ethiopia, Senegal, na Peru, utaboresha sekta ya utengenezaji bidhaa hapa nchini kwa kuwekeza zaidi ya dola bilioni 30 za Marekani kwenye sekta hiyo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Also Read
Rais ataka sheria zitakazofanikisha ajenda nne kuu za serikali kupewa umuhimu

Kwenye hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mpango huo kwa njia ya video, Rais Uhuru Kenyatta alisema Kenya iliamua kuzindua mpango huo ili kuimarisha ustawi wa kiviwanda hapa nchini.

Kwenye hafla hiyo ambayo pia ilihutubiwa na mkurugenzi mkuu wa shirika la UNIDO Li Yong, Rais Kenyatta alitangaza kuwa kamati ya utekelezaji wa Maendeleo ya kitaifa na mawasiliano inayoongozwa na waziri wa usalama wa kitaifa Dr. Fred Matiang’i itasimamia uatekelezaji wa mpango huo hapa nchini.

Also Read
Rais Kenyatta ndiye mwenyekiti mpya wa Jumuia ya Afrika Mashariki

Natoa agizo kwa waziri wa usalama wa kitaifa, waziri wa fedha Ukur Yatani na yule wa biashara, kutoa mwongozo ili kufanikisha mpango wa PCP sawia na kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali za utekelezwaji wake,” aliagiza rais.

Also Read
Watu watatu zaidi wafariki kutokana na Covid-19 hapa nchini

Akiongea kutoka mjini Geneva Uswizi,Li Yong alitangaza mpango wa shirika lake wa kusaidia Kenya katika kutekeleza mpango wake wa ufufuzi wa uchumi baada ya janga la Covid 19.

Mbali na kuimarisha sekta ya utengenezaji bidhaa, Li Yong alisema mpango huo pia utakuza uchumi wa dijitali wa nchi hii na kuboresha hadhi ya taifa hili kama nchi hiyo iliyostawi zaidi katika kanda ya Afrika Mashariki.

  

Latest posts

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Serikali yaongeza kafyu ya kuto-toka nje usiku katika kaunti tatu za Rift Valley

Tom Mathinji

Karua asema Muungano wa Azimio utahakikisha uongozi bora

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi