Mpiga rekodi wa Mombasa Nicky Phondo aaga dunia

Mcheza muziki uliorekodiwa au ukipenda DJ wa Mombasa kwa jina Nicky Phondo ameaga Dunia. Dj Nicky, anasemekana kufa kwenye ajali mbaya ya barabarani ijumaa tarehe 18 mwezi Disemba mwaka huu wa 2020 akielekea nyumbani kutoka kazi ya usiku.

Inaaminika kwamba alikuwa amekwenda kucheza muziki kwenye tukio fulani la usiku ambalo halijajulikana.

Wasanii wa Mombasa kama vile Madebe na Gates Mgenge ndio walithibitisha kifo cha Dj Nicky kwenye mitandao ya kijamii.

Eneo la ajali halijajulikana lakini picha za gari baada ya ajali zinaonyesha kwamba ilikuwa ajali mbaya. Duru zinaarifu kwamba Dj Nicky aliaga dunia siku moja tu baada ya kuadhimisha miaka 35 tangu kuzaliwa.

Also Read
Wakazi wa Jomvu, Mombasa wahimizwa kuzingatia kanuni kuhusu COVID-19

Mwaka huu wa 2020 umeshuhudia vifo vya watu wengi maarufu nchini Kenya, wakiwemo wale wa sekta ya sanaa na burudani.

Mchekeshaji Ben Maurice Onyango maarufu kama Othuol Othuol aliaga dunia mwezi Oktoba mwaka huu wa 2020 katika hospitali kuu ya Kenyatta jijini Nairobi ambako alikuwa amelazwa kwa siku kadhaa kutokana na uvimbe kwenye ubongo.

Also Read
Matatizo ya kiakili ya Chacha ni ya dhulma kwenye ndoa yake, Victoria Inyama.

Muigizaji Charles Bukeko ambaye wengi walimjua kama Papa Shirandula aliaga dunia mwezi wa sita mwaka huu kutokana na kile kinachosemekana kuwa Covid 19.

Alikata roho akiwa ndani ya gari kwenye maegesho ya magari katika hospitali moja ambako alikuwa amekimbizwa na mke wake baada ya kuhisi vibaya.

Mchekeshaji Kasee naye alituacha mwezi huo wa sita baada ya mwili wake kusemekana kupatikana kando ya barabara iliyokuwa ikielekea kwenye makazi yake.

Also Read
Ringtone afika mahakamani akiwa kwenye Ambulensi

Lady Maureen ambaye wengi walimkubali kama malkia wa muziki aina ya Ohangla wa lugha ya kijaluo aliaga dunia mwezi Julai mwaka huu wa 2020 nyumbani kwao katika kaunti ya Migori baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Wengine ni Abeny Jachiga mwanamuziki wa Ohangla, Kasongo wa Kanema mwanamuziki wa Rhumba, Rhino Kaboom aliyekuwa akiimba kwa lugha ya kikalenjin, Jimmy Wayuni wa muziki wa lugha ya Kikuyu kati ya wengine wengi.

  

Latest posts

Wasanii Wanaowakilisha Kenya AFRIMA

Marion Bosire

Akothee Apata Mgeni wa Heshima Kwenye Hafla Yake

Marion Bosire

KFCB Yazuia Usambazaji Wa Filamu

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi