Mr. Macaroni aachiliwa kwa dhamana

Mchekeshaji na muigizaji wa nchi ya Nigeria Debo Adebayo maarufu kama Mr. Macaroni aliachiliwa kwa dhamana ya Naira Laki moja, baada ya kukamatwa kwenye lango kuu la mji wa Lekki katika jimbo la Lagos nchini Nigeria siku mbili zilizopita.

Macaroni na watu wengine 32 walikamatwa asubuhi ya Jumamosi tarehe 13 mwezi Februari mwaka huu wa 2021 kwa kutekeleza maandamano katika eneo hilo kulalamikia mauaji ya watu waliokuwa wakiandamana katika eneo hilo hilo mwezi Oktoba mwaka 2020.

Also Read
Stephanie Okereke Linus ateuliwa balozi wa usafi wa mazingira Nigeria.

Macaroni alifika katika eneo hilo na kuanza kuonyesha matukio mubashara kupitia akaunti yake ya Instagram ndipo akakamatwa. Aliendeleza video hiyo akionyesha hadi anapoingizwa kwenye gari la polisi.

Watu wengi maarufu nchini Nigeria kama vile waigizaji walilalamikia kukamatwa kwa muigizaji huyo na wengine ambao walikuwa kwenye maandamano. Reno Omokri ambaye ni mwandishi wa vitabu na mwanasiasa alijitolea kulipa wakili kwa niaba ya Macaroni.

Kamishna wa polisi katika Jimbo la Lagos, Hakeem Odumosu alitangaza jumamosi kwamba Macaroni na wengine waliokamatwa naye walistahili kuachiliwa kwa dhamana mara moja.

Macaroni alipoachiliwa jana, alijulisha wafuasi wake wote kupitia video kwenye Instagram huku akishukuru wote waliozungumza kuhusu kukamatwa kwao.

Kulingana naye hatua ya wengi kuzungumzia kukamatwa kwao ilisaidia kwani wengi wangeuawa.

  

Latest posts

Mwelekezi Sir Jacob Otieno Ameaga Dunia

Marion Bosire

Daddy Owen Azindua Albamu Mpya

Marion Bosire

Ogopa Wasanii, Kibao Kipya Cha Willy Paul

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi