Mr. Seed Asimulia Safari Yake ya Muziki

Moses Tarus Omondi maarufu kama Mr Seed alikuwa mgeni wetu asubuhi ya Leo kwenye kipindi cha Good Morning Kenya ambapo alisimulia safari yake ya muziki.

Alihojiwa na Doreen Arange ambapo Mwimbaji huyo wa nyimbo za injili za kisasa alisema alianza kuimba akiwa na umri mdogo kama mwanafunzi na aliamua kutafuta ushirikiano na wanamuziki ambao tayari walikuwa wanafanya vyema.

Alishirikishwa na Kundi la MoG yaani Men of God kwenye wimbo uitwao “Papa God” ambapo mtindo wake wa kuimba ulikuwa wa asili ya Nigeria. Wengi walidhania yeye ni mzaliwa wa Nigeria.

Also Read
Kapedo Aelezea alivyoathirika na Janga La Corona

Mahojiano yake ya kwanza yalikuwa ya jarida la Insyder na Bi. Tamima ambaye pia alikuwa akimpa nafasi ya kuimba kwenye mikutano ya shule za upili.

Watangazaji wa kituo cha redio cha Kiss Kalekye Mumo na Shaffie Weru pia walichangia ukuaji wa Mr. Seed kwenye muziki baada ya kuamua kumtambua binafsi kila walipocheza kibao cha Papa God.

Also Read
Safari ya kwenda AFCON 2021 yarejea

Mr Seed alichukua mapumziko ya miaka miwili kutoka kwa muziki baada ya kuhusu kwamba alikuwa anafanya bidii lakini nyota yake ilikuwa haing’ai. Alipata msongo wa mawazo lakini anashukuru marafiki wake wa karibu ambao walimsaidia kuendelea. Anashukuru pia mke wake Nimo ambaye anasema alikuwa akimpelekea chakula na hata kumsaidia kulipa ada ya nyumba.

Baada ya miaka miwili, Mr. Seed alirejea na kibao ‘Kumbe kumbe’ ambacho anasema alikuwa nacho hata kabla ya mapumziko.

Also Read
Je,unayafahamu majukumu ya vikosi vya ulinzi vya Kenya-KDF?

Kibao hicho kilifufua ari yake ya kuwa mwanamuziki bora na tangu wakati huo hajaangalia nyuma.

Kuhusu albamu yake ya “The Black Child” alisema alikuwa na nyimbo kama 20 lakini akachagua kumi tu. Alishauri waimbaji hasa wanaoanza sasa wawe na subira na wajitolee kabisa.

Alifichua kwamba unaweza kuwekeza pesa nyingi kwenye kazi ya muziki na ukose kupata lolote baadaye.

  

Latest posts

Shona Ferguson Ashinda Tuzo Hata Baada Ya Kifo

Marion Bosire

Snoop Dogg Atangaza Kifo Cha Mamake

Marion Bosire

Etana Kutumbuiza Nairobi

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi