Mrisho Mpoto Asema Anataka Kupunguza Wapumbavu Tanzania

Mwanamuziki wa Tanzania Mrisho Mpoto amesema kwamba yuko kwenye safari ya kupunguza wapumbavu nchini Tanzania nchi hiyo ibakie na wajinga tu. Kulingana naye mpumbavu hasaidiki lakini mjinga anaweza kuelimishwa.

Akihojiwa kuhusu wimbo wake wa hivi punde kwa jina “Tausi” ambao amemhusisha Mbosso kutoka Wasafi WCB, Mpoto alisema kwamba yeye anapenda sana kutumia akili na kufikiria mambo ya ndani. Miaka 60 tangu nchi hiyo ijipatie uhuru Mpoto anasema kwamba bado watanzania hawajajikita kwenye utaifa wao.

Also Read
Cicely Tyson ameaga dunia

Alizungumza kuhusu sekta ya muziki nchini humo ambayo anasema imeingiliwa na upumbavu kwa vile wanamuziki nchini humo wanakimbilia mitindo ya muziki ya nchi zingine na kusahau kuendeleza mitindo ya kwao. Alitaja mtindo wa Afrika Kusini Amapiano, mtindo wa Nigeria, wa Congo na nchi nyingine. Anasema wanamuziki tajika wa Tanzania wanafikiria sana kuhusu nyimbo ambazo zitawapa mapato na kusahau nyimbo za kitanzania.

Also Read
Rais wa Tanzania amshtumu mbunge anayepinga chanjo dhidi ya COVID-19
Also Read
Miaka mitano gerezani kwa AmberRutty, Said na James au faini ya milioni 11!

Mrisho Mpoto ambaye alihusika kwenye ajali ya barabarani hivi maajuzi anadhamiria kurai wanamuziki wenzake nchini Tanzania warejelee mitindo yao ya muziki na kuisukuma kama ajenda jinsi nchi zingine zinafanya. Wimbo huo Tausi anasema ni wa kukumbusha wanamuziki wenzake waimbe nyimbo kitanzania.

  

Latest posts

Rais Samia Alivyosherehekewa Kwenye Siku Yake ya Kuzaliwa

Marion Bosire

Azimio la Bien Barasa Mwaka Huu

Marion Bosire

Anne Kansiime Afiwa na Baba Mzazi

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi