Mshindi wa Urais katika uchaguzi mkuu wa Jumanne kubainika katika raundi ya kwanza

Mchanganuzi wa siasa ambaye pia ni mwenyekiti wa shirika la Pan Africa UK Ltd ,Dkt David Matsanga amesema kuwa ana imani ya uchaguzi mkuu wa jumanne kumalizika katika raundi ya kwanza na kuondolea uwezekano wa kuingia raundi ya pili .

Akizungumza na Radio Taifa,  Dkt Matsanga amesema kulingana na hali ilivyo huenda Raila Odinga akapata kati ya asilimia 51 hadi 55 ya kura zote na kushinda kinyang’anyiro  cha ikulu katika raundi ya kwanza dhidi ya mpinzani wa karibu William Ruto.

Also Read
Sonko adinda kuondoka kituo cha IEBC baada ya tume hiyo kukataa kumwidhinisha

Pia Matsanga amezungumzia kuhusu  hotuba za mikutano ya mwisho ya kampeini siku ya jumamosi akiukosoa muungano wa Kenya kwanza unaongozwa na Ruto kwa kuzingatia zaidi matusi dhidi ya Rais badala ya kuuza sera  na kuipongeza pia hotuba ya kinara wa Azimio ,Odinga kuwa ya kishujaa na uzalendo iliyoashiria kuwa tayari kukubali matokeo ya uchaguzi.

Also Read
Uchaguzi wa Mbunge Wasimamishwa Katika Eneo Bunge la Kitui Rural

Matsanga ameelezea kuwa uchaguzi wa Kenya utaathiri ukanda wa Afrika mashariki kwa vovyote kwani endapo kutakuwa na vurumai au msukosuko wa uongozi  mataifa mengi ya Afrika mashariki yataathirika kibiashara na kimaendeleo kwani Kenya Kenya inategemewa pakubwa.

Also Read
Watu sita wafariki katika ajali ya barabarani Loitoktok

Wakenya milioni 22 na uhei waliojiandikisha watashiriki zoezi la kupiga kura kote nchini ,ambapo kila mpiga kura atakuwa na fursa ya kuwachagua viongozi sita,Rais,Gavana,Seneta,Mbunge,Mwakilishi wa akina mama na mwakilishi wadi.

  

Latest posts

Maendeleo ya Wanawake yampongeza Rais kwa kuwateuwa wanawake mawaziri

Dismas Otuke

NMS yakabidhi majukumu yake kwa kaunti ya Nairobi

Tom Mathinji

Hamisi Massa ateuliwa kaimu Mkurugenzi wa idara ya DCI

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi