Mshukiwa wa mauaji ya watu watano wa familia moja Kiambu aungama

Maafisa kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) sasa wanachunguza ushahidi ili kutegua kitendawili cha mauaji ya kinyama ya watu watano wa familia moja katika Kaunti ya Kiambu.

Hii ni baada ya mwanaume mwenye umri wa miaka 22, anayefahamika kama Lawrence Simon Warunge, kukamatwa kuhusiana na mauaji hayo na kuanza kutoa habari muhimu kwa maafisa hao.

Also Read
KeNHA yakabili msongamano wa magari unaosababishwa na ujenzi wa barabara ya moja kwa moja Nairobi

Kulingana na maafisa wa DCI, Warunge sasa ndiye mshukiwa mkuu wa uhalifu huo ambapo watu watano kutoka familia moja katika Kijiji cha Kagongo waliuawa kinyama.

Warunge alikamatwa pamoja na mwanamke mmoja anayesemekana kuwa mpenziwe siku ya Jumamosi kutoka mafichoni katika eneo la Kabete ya Chini, Kaunti ya Kiambu na wawili hao sasa wanazuiliwa na polisi.

Also Read
Somalia yafungua tena ubalozi wake Jijini Nairobi

Warunge aliwaongoza maafisa wapelelezi hadi kwenye shimo la choo ambamo alitumbukiza silaha zinazoaminika kutumika katika mauaji hayo katika eneo la Mai Mahiu.

Kulingana na Idara ya DCI, silaha hizo zilizopatikana zitafanyiwa uchunguzi zaidi wa kimaabara ili zitumike kama ushahidi mwafaka wa kuwafungulia mashtaka washukiwa wa kitendo hicho.

Also Read
Mtu mmoja auawa na fisi, watatu wajeruhiwa huko Samburu

Wapelelezi wanaamini kwamba waliotekeleza mauaji hayo ni watu wanaofahamika vizuri na familia hiyo, kwani hakuna ishara yoyote kwamba waliingia katika boma hilo kwa nguvu.

Kisa hicho kiliwaacha majirani na wakazi wa eneo hilo vinywa wazi.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi