“Msifananishe binti yangu na Chloe!” asema Matthew Knowles

Babake msanii wa muziki nchini Marekani Beyonce anayefahamika kama Matthew Knowles ameonyesha kutoridhika na maoni ya watu kadhaa ambao wanafananisha binti yake Beyonce na mwimbaji kwa jina Chloe.

Matthew wa umri wa miaka 69 sasa alikuwa akizungumza kwenye mahojiano na Bi. Leah A. Henry kwenye kipindi chake cha mitandaoni kiitwacho “Lemonade Stand”.

Also Read
Kambua aomboleza kifo cha mtoto wake

Bi Leah alitaka kusikia maoni ya Knowles kuhusu maoni ya mashabiki wa kina dada wawili Chloe na Halle ambao wanahisi kwamba Chloe anafanana na Beyonce hata kwenye kiwango cha talanta ya uimbaji.

Hapo ndipo mzee huyo alipandwa na hasira na kurejelea mashabiki hao kama “wajinga” yaani “idiots”. Kulingana naye, Chloe anaweza kuigiza kama Beyonce ikiwa atahitajika kufanya hivyo kwenye filamu ya maisha ya Beyonce lakini talanta yake yaijafikia ile ya Beyonce.

Also Read
Solanje Knowles asema alikuwa akiugua huku akitayarisha muziki
Chloe Bailey

Kina dada hao wawili Chloe na Halle ni wanamuziki na wanafanya kazi pamoja kama kundi na wamesajiliwa na Beyonce kwenye kampuni yake ya kusimamia wanamuziki tangu mwaka 2018.

Chloe X Halle

Mzee huyo ambaye amefanya kazi kama meneja wa talanta hasa za muziki kwa miaka mingi anahisi kwamba Barbra Streisand ndiye yuko kiwango sawa na Beyonce.

Also Read
Kamala Harris aongoza watu wengine mashuhuri kumkumbuka George Floyd

Bwana Matthew ndiye alikuwa meneja wa wasanii wa kundi la Destiny Child ambapo Beyonce alikuwa mmoja wao na amesimamia binti zake Beyonce na Solanje ambao kila mmoja anaimba kivyake.

  

Latest posts

Rayvanny Kumtambulisha Msanii wa Kwanza NLM

Marion Bosire

Dulla Makabila Ajiondolea Lawama

Marion Bosire

Mwigizaji Atoa Ilani Kwa Rais Museveni

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi