Msongamano wa wanafunzi wakumba shule za Upili kaunti ya Bungoma

Shule za upili katika Kaunti ya Bungoma zinakabiliwa na msongamano kutokana na shinikizo kwa shule hizo kusajili idadi kubwa ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza ili kufanikisha mpango wa wanafunzi wote waliokamilisha masomo ya msingi kujiunga na zile za upili.

Utafiti uliofanywa na Shiirika la Habari nchini katika kaunti ya Bungoma, ulibaini kuwa wakuu wengi wamegeuza maabara na majengo ya maktaba kuwa vyumba vya madarasa na mabweni ili kukabiliana na idadi kubwa ya wanafunzi.

Also Read
Afisa wa GSU amuua mwenzake kwa kumpiga risasi kaunti ya Laikipia

Mkuu wa Shule ya Upili ya St Mary’s Kibabii, Nicodemus Ogeto, aliiambia shirika hilo kwamba licha ya Wizara ya Elimu kutengea shule hiyo nafasi 499 za wanafunzi, shule hiyo imesajili wanafunzi 690.

Also Read
Spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi ajiunga na muungano wa Kenya Kwanza

Ogeto alisema shule hiyo haina mabweni na vyumba vya madarasa vya kutosha ambavyo vinaweza kuchukua idadi kubwa ya wanafunzi ambayo sasa ni jumla ya wanafunzi 1,960.

Kadhalika alisikitishwa na uhaba mkubwa wa walimu shuleni humo na akatoa wito kwa Tume ya Kuajiri Walimu Nchini (TSC) kuajiri walimu zaidi.

Also Read
Wizara ya Afya yabadilisha mwongozo wa shughuli za mazishi

Shule hiyo ina walimu 55 wa Tume ya Kuajiri walimu TSC, na walimu saba wameajiriwa na  halmashauri inayoisimamia huku, wawili wakiwa chini ya Mpango wa uanagenzi.

  

Latest posts

Japhet Koome ateuliwa Inspekta Jenerali wa Polisi

Tom Mathinji

Majukumu ya Naibu Rais Rigathi Gachagua yabainishwa

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi ateuliwa waziri mwenye Mamlaka zaidi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi