Mtaala wa CBC umekosa uhamasishaji wa wadu husika yesema KUPPET

Chama cha walimu wa shule za sekondari na vyuo  nchini Kenya KUPPET kimeikosa wizara ya michezo kwa kushindwa kufanaya uhamasishaji wa wadau kabla ya utekelezaji wa mtaala mpya wa elimu wa CBC.

Akello Misori katika mahojiano kupitia Idhaa ya kimombo

Akizungumza na KBC katibu mkuu wa KUPPET Akelo Misori amesema  hakuna kampeini ya kupinga mtaala huo,ila  wizara ya elimu  na tume ya kuwaajiri walimu TSC , haijawahamasisha  wadau  kikamilifu .

Also Read
Mabunge 10 ya kaunti eneo la Mlima Kenya kuunga mkono BBI

“Sikubaliani  kuwa kuna kampeini ya kipinga CBC,kitu kimekosana na Walimu kuhamasishwa na kupewa uwezo wa kuwafundisha wanafunzi sahihi kuhusu  mtaala huo,TSC inapaswa kuainisha mipangilio yake ili  walimu wanaoendesha mtaala huo wapewe uwezo na kubadilisha nia na  pili kukumbatia mbinu zinazofunzwa kupitia mtaala huu”akasema Misori

Also Read
Shule zafunguliwa kote nchini kwa mwaka mpya wa masomo wa 2021

Mtaala mpya wa Elimu  wa CBC ulioanza kutekelezwa miaka minne iliyopita ,  unaopendekeza  wanafunzi  kusoma shule ya msingi kwa miaka  miwili katika shule ya chekechea ,miaka 6 katika shule ya msingi  ,miaka mitatu katika shule ya sekondari na miaka mitatu katika chuo kikuu( 2-6-3-3) .

Also Read
KUPPET yapinga hatua ya kusitishwa nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma

Hata hivyo mtaala huo umepokea pingamizi kutoka  wadau wengi wakiwemo,wazazi kwa kukosa mwelekeo ufaao ,wengi wakiona kuwa unapotosha,ingawa wizara ya Elimu imesimama kidete kuwa haitbadilisha mtaala huo.

  

Latest posts

Idadi ndogo ya wakazi wa Nairobi wajitokeza kuchanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 200,000 za Sinopharm kutoka China

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi