Muda wa kafyu waongezwa huku mikutano ya hadhara ikipigwa marufuku

Waziri wa afya Mutahi Kagwe ametangaza kuongezwa kwa muda wa kafyuu kote nchini alisema kafyu itaanza saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri kote nchini.

Waziri Kagwe alisema mikusanyiko yote ya umma imeahirishwa kufuatia kuongezeka visa vya maambukizi ya COVID-19 humu nchini.

Also Read
Kiwango cha maambukizi ya COVID-19 hapa nchini ni cha asilimia 8.1

Akihutubia taifa siku ya Ijumaa katika jumba la Harambee, Waziri huyo alidokeza kuwa mikutano kadhaa ya serikali pia imeahirishwa.

Waziri huyo aliwahimiza waajiri kuwaruhusu wafanyikazi kufanyia kazi nyumbani kulingana na haja ilivyo.

Aidha Kagwe alisema visa vya maambukizi vimeongezeka katika kaunti za Kiambu, Kajiado, Lamu, Makueni Muranga, Taita Taveta na kwa mara ya kwanza katika kaunti ya Tana River.

Also Read
Rais Kenyatta: Covid-19 imeathiri ajenda ya kimataifa ya kuwawezesha vijana

Aliagiza kwamba sehemu za ibada ziwe na thuluthi moja ya idadi ya kawaida ya waumini kwa uzingativu kikamilifu kanuni za kuzuia msambao wa COVID-19 huku waumini wakitakiwa kuwa umbali wa angalau mita moja.

Also Read
Baraza la madhehebu mbali mbali laongezewa muda wa kuhudumu

Mikahawa na sehemu za lishe zimetkiwa kuendesha shughuli zao kulingana na kanuni zilizowekwa na wizara ya afya.

Wakati huo huo Kenya inatarajiwa kupokea dozi 400,000  za chanjo ya AstraZeneca kutoka kwa serikali ya Uingereza.

  

Latest posts

Nabulindo ashinda kesi ya kupinga kuchaguliwa kuwa mbunge wa Matungu

Dismas Otuke

Chama cha Social Democrats chatwaa ushindi nchini Ujerumani

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa vilivyopungua zaidi vya Covid-19

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi