Mudavadi anyemelea kura za eneo la Mlima Kenya

Kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi amefanya kikao cha mashauriano na Gavana wa Kaunti ya Kirinyaga Ann Waiguru katika harakati za kutafuta uungwaji mkono katika eneo la Mlima Kenya kwenye azma yake ya kuwa rais.

Mudavadi, ambaye ametangaza kuwa hataunga mkono mgombea mwengine yeyote wa urais mwaka wa 2022, anajaribu kuwarai viongozi na wakazi wa eneo hilo lenye kura nyingi ili wamuunge mkono yeye.

Waiguru anasema wawili hao walizungumzia na kuelewana kuhusu umoja wa kitaifa, maswala ya kiuchumi, afya na ujumuishaji wa wanawake katika uongozi wa serikali.

Also Read
Acha kuniiga, Gavana Alred Mutua amwambia Musalia Mudavadi

Kikao chake na Waiguru kinajiri siku chache tu baada ya kualikwa na baadhi ya wabunge wa zamani wa eneo hilo huko Sagana ambako walizungumzia jinsi ya kushirikiana kwa ajili ya matayarisho ya uchaguzi mkuu ujao.

Kwenye kikao hicho cha Sagana, kilichoandaliwa na waliokuwa wabunge Mutava Musyimi na Humphrey Njuguna, Mudavadi alisema kuwa anaomba uungaji mkono wa eneo hilo ili amrithi Rais Uhuru Kenyatta wakati atakapostaafu.

Also Read
Mwakilishi Wadi ya Muguga Eliud Ngugi afariki kutokana na COVID-19

“Nahitaji ushirikiano wenu na maombi yenu. Eneo hili la Mlima Kenya lina umuhimu mkubwa na haliwezi kuachwa nje na yeyote anayehitaji kuongoza nchi hii. Mchango wenu, juhudi na baraka zenu kama eneo vitakuwa na umuhimu mkubwa sana katika safari yangu,” akasema Mudavadi.

Njuguna aliunga mkono pendekezo la Mudavadi na kuahidi kuendelea kushirikiana naye, akihoji kuwa eneo la Mlima Kenya lina idadi kubwa ya kura zinazoweza kuamua matokeo ya uchaguzi wa urais mwaka ujao.

Also Read
Musalia Mudavadi: Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022 haupaswi kuahirishwa

Kwa upande wake Musyimi alielezea kufurahishwa na mazungumzo waliyokuwa nayo na Mudavadi, akisema maswala yaliyojadiliwa ndiyo yanayoathiri wananchi.

Wiki moja kabla kikao cha Sagana, Mudavadi alizuru eneo bunge la Kieni katika Kaunti ya Nyeri ambako alishirikiana na mbunge wa eneo hilo Kanini Kegan a viongozi wengine wakiwemo mawaziri Mutahi Kagwe, Joe Mucheru, Peter Munya na Gavana Mutahi Kahiga.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi