Mulamwah Akaribisha Mwanawe

Mchekeshaji David Oyando maarufu kama Kendrick Mulamwah ametangaza kuzaliwa kwa binti yake kwa jina Keilah Oyando. Alitangaza hayo kupitia kwa akaunti zake za mitandao ya kijamii huku akimshukuru mke wake Carol Sonnie kwa kuvumilia matatizo yote ya ujauzito.

Mulamwah alishukuru pia mashabiki na marafiki ambao alisema wamekuwa wakiwaombea wapate salama. Anasema mwanao ana sura ya kuvutia na anasubiri siku ambayo ataonyesha sura yake kwa umma.

Also Read
Mange Kimambi Afunguka Mazito Kuhusu Ali Kiba

Mwanzo wa mwezi Agosti mwaka huu, mchekeshaji huyo alimtakia mpenzi wake Carol Sonnie kila la heri anapokwenda kujifungua mtoto wao wa kwanza.

Wakati huo alikiri mapenzi aliyonayo kwa mama na mtoto mtarajiwa akitaja safari ndefu ambayo wamepita hadi sasa.

Also Read
Amber Rutty asema atashirikiana na Chris Brown kwenye kibao!

Alishukuru Sonnie kwa kubeba mwanao kwa muda huu wote na kumtakia mema maishani na katika taaluma yake.

Mulamwah na Carol waliwahi kutengana kwa muda baada ya ujauzito wao wa kwanza kuharibika ukiwa miezi mitatu.

Baadaye tena alichoma shati lake ambalo huwa analitumia kama sare ya kuigiza na kutangaza kwamba ameachana na fani ya uchekeshaji. Alilaumu mashabiki kwa kuharibika kwa ujauzito wa mpenzi wake wakati huo akisema walimsababishia msongo wa mawazo.

Also Read
Vanessa Mdee achumbiwa na Rotimi

Walitangaza kutengana kwao mwezi Oktoba mwaka 2020 na Januari mwaka huu wa 2021 wakatangaza kwamba wamerudiana.

Wawili hao sasa wamepata mtoto wao wa kwanza.

  

Latest posts

Ogopa Wasanii, Kibao Kipya Cha Willy Paul

Marion Bosire

Kipindi Cha Wendy Williams Kuendelezwa na Watangazaji Tofauti

Marion Bosire

“Upendo” Kibao Kipya Kutoka Kwa Zuchu Na Spice Diana

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi