Mulee ana imani Kenya kuwashinda Misri na Togo

Kocha wa Harambee stars Jacob Ghost Mulee ana imani kuwa wataandikisha historia upya na kuwashinda Misri kwa mara ya kwanza Alhamisi hii katika mchuano wa kundi G kufuzu kwa kombe la AFCON mwaka ujao.

Mulee amesema wamejiandaa vyema kwa mchuano huo ambapo  analenga kuwatumia wachezaji chipukizi na wengi wanaochez soka humu nchini wanapojiandaa kwa mechi za kufuzu kwa kombe la dunia kuanzia mwezi Juni mwaka huu.

Also Read
Casa Mbungo atua Bandarini kupiga ukufunzi kwa miaka miwili

“Mimi nina imani tuko sawa na hata kama hatujawahikuwashinda Misri,lakini tuna uwezo wa kuvunja rekodi tuwashinde kisha tuakienda Togo pia tupatae ushindi,bado kunayo matumaini ya kufuzu kwenda Cmeroon mwaka ujao,pia nitatumia mechi hizo  kama matayarisho ya mechi za kufuzu kombe la dunia kuanzia mwezi Juni”.

Also Read
Gor Mahia wazimwa nyumbani na wageni NAPSA All Stars kutoka Zambia

Mulee amesema hayo Jumanne wakati wa dhifa ya chakula cha mchana iliyoandaliwa kwa timu ya taifa na kampuni ya Odi Bets.

Also Read
Malawi yafuzu kwa fainali za AFCON kwa mara ya 3 baada ya kuwabwaga Uganda Cranes 1-0

Kenya ni ya tatu kundi G la kufuzu kwa pointi 3 ,nyuma ya Misri na Comoros walio na alama 8 kila moja.

 

  

Latest posts

Police Fc washerehekea kurejea ligi kuu baada ya mwongo mmoja kwa dhifa

Dismas Otuke

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi