Mung’ara Githinji wa Jubilee ashinda uchaguzi mdogo wa Wadi ya Mugugua

Mgombea wa chama cha Jubilee Mung’ara Joseph Githinji ameshinda kiti cha Mwakilishi Wadi ya Mugugua.

Hii ni baada ya kupata jumla ya kura 4,089, ambayo ni takribani asilimia 50 ya kura zote zilizopigwa katika uchaguzi mdogo huo uliofanyika Alhamisi.

Kwa mujibu wa matokeo kutoka kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini IEBC, Mgombea wa chama cha UDA Peter Thumbi, aliyeungwa mkono na Naibu Rais William Ruto, ameibuka wa pili kwa kura 4,062.

Also Read
IEBC yatangaza tarehe ya chaguzi ndogo za Garissa, Bonchari na Juja

Kufuatia ushindi huo, Mung’ara amewashukuru wakazi wa Wadi ya Muguga kwa kujitokeza kwa wingi na kutekeleza haki yao ya kikatiba na kwa kumuunga mkono hadi akapata ushindi huo.

Also Read
Tume ya IEBC yapinga mapendekezo ya BBI

Wakazi wengi walijitokeza ili kushiriki katika zoezi hilo la uchaguzi mdogo, lililoshuhudia zaidi ya asilimia 45 ya wapiga kura kujitokeza.

Wagombea wengine katika kinyang’anyiro hicho walikuwa ni Mumbi Moses Gichau wa chama cha Thirdway Alliacne aliyepata kura 49 na Mugo Peter Njoroge wa chama cha Peoples Party of Kenya (PPK) ambaye alipata jumla ya kura 32.

Also Read
Mudavadi ajitosa rasmi ulingoni huku mwangwi wa BBI ukivuma kote nchini

Nafasi hiyo iliachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwakilishi Wadi ya Mugugua Eliud Ngugi.

  

Latest posts

ODM yashutumu vikali ghasia za Migori dhidi ya Jimi Wanjigi

Tom Mathinji

Prof. Magoha: Mtaala mpya wa elimu hautatupiliwa mbali

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi