Munya apuuzilia mbali kutawazwa kwa Spika Muturi kuwa msemaji wa Mlima Kenya

Waziri wa Kilimo Peter Munya amepuuzilia mbali kutawazwa kwa Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi, kuwa msemaji wa eneo la Mlima Kenya.

Waziri Munya amehoji kuwa wadhifa huo hauna umuhimu wowote na wala hakuna afisi ya msemaji mahali popote.

Akiongea huko Isiolo alipokutana na wakazi wa Kaunti za Meru na Isiolo wanaotishiwa kufurushwa, Munya alisema hajafahamu majukumu ya msemaji wa jamii.

Also Read
Musalia Mudavadi: Rais Kenyatta hanipigii debe kuwa mridhi wake

Munya alisema eneo la Mlima Kenya liko nyuma ya Rais Uhuru Kenyatta na ni yeye atakayetoa mwongozo kuhusu mwelekeo wa kisiasa katika eneo hilo kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Kutawazwa kwa Muturi kumeungwa mkono na magavana Kiraitu Murungi wa Meru, Martin Wambora wa Embu na Muthomi Njuki wa Tharaka Nithi, lakini kukapingwa na Gavana wa Murang’a  Mwangi Wa Iria na mwenzake wa Kirinyaga, Anne Waiguru.

Also Read
Muturi: Sibanduki katika kinyang'anyiro cha kuwania Urais

Spika Muturi jana alitawazwa kuwa msemaji wa kisiasa wa eneo la Mlima Kenya, kwenye sherehe iliyoandaliwa katika Hekalu la Mukurwe wa Nyagathanga huku kukiwa na wasi wasi wa kuvurugwa kwa sherehe hiyo na watu wanaopinga tambiko hilo.

Licha ya vitisho vya kuvurugwa kwa sherehe hizo kutoka kwa Gavana wa Kaunti ya Muranga Mwangi wa Iria, aliyepinga sherehe hiyo, wazee wa jamii za Kikuyu, Meru, Embu na Mbeere walianza kuwasili kwa sherehe hizo mapema.

Also Read
Kenya yajiandaa kukabiliana na wimbi la pili la uvamizi wa nzige

Sherehe hizo zilichukua muda wa zaidi ya masaa mawili na picha hazikuruhusiwa kuchukuliwa.

Waliopinga sherehe hizo walidai kwamba kutawazwa kwa Muturi lilikuwa jaribio la kumdunisha Rais Uhuru Kenyatta kama kiongozi wa eneo hilo.

  

Latest posts

Wateja Milioni nne wa Fuliza kuondolewa kutoka CRB

Tom Mathinji

Watu watatu wafariki kutokana na Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Rais Ruto: Serikali kudhibiti vilivyo makali ya njaa hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi