Murathe na Gachoka wapata wakati mgumu mbele ya bunge wakijitetea kuhusu sakata ya KEMSA

Naibu Mwenyekiti wa chama cha Jubilee David Murathe amehojiwa na wabunge kuhusu sakata ya KEMSA ya fedha za kukabiliana na COVID-19.

Kamati ya Bunge kuhusu uwekezaji wa umma ikiongozwa na Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir, ilimtaka Murathe kufika mbele yake kutoa maelezo kuhusu madai ya kuhusika kwake katika sakata hiyo.

Kampuni ya Kilig Limited, ambayo inahusishwa na Murathe, ilikabidhiwa zabuni ya shilingi bilioni 4 kusambaza vifaa vya kujikinga na virusi vya korona kwa Halmashauri ya usambazaji Dawa (KEMSA).

Also Read
Wananchi wafaa kuongeza juhudu dhidi ya Covid-19

Mbunge wa Wajir Mashariki Rashid Amin amesema kukiri kwa Murathe kuwa muhusika mkuu wa akiba ya kampuni hiyo katika Benki ya Equity ni ishara tosha kwamba alitumia ushawishi wake kisiasa kupata zabuni hiyo kupitia kampuni hiyo isiyo na umaarufu.

Also Read
Watu 390 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Akijitetea, Murathe alisema kampuni ya Kilig ilimuomba kuwa mmoja wa wakurugenzi wake ili kuiwezesha kupata zabuni hiyo ya kusambaza vifaa kinga.

Aidha, Murathe alisema alijiondoa kwenye kampuni hiyo mara tu KEMSA ilipofutilia mbali mpango wa kutoa zabuni hiyo kwa kampuni hiyo kutokana na uhaba wa fedha.

Baadaye kamati hiyo pia ikamhoji aliyekuwa mmiliki wa kampuni hiyo iliyosajiliwa mwaka jana Januari, Wilbroad Gachoka, kuhusiana na sakata hiyo.

Also Read
Baadhi ya wanawake wakataa BBI

Gachoka pia amekana madai ya kuhusika katika sakata hiyo na kusema kwamba aliuza kampuni hiyo siku chache baada ya kupewa zabuni hiyo.

Hata hivyo, Gachoka amekiri kwamba badi ni mweka-sahihi kwenye akaunti ya benki ya kampuni hiyo, licha ya kudai kuwa aliiuza.

  

Latest posts

Justin Muturi kuwania urais kwa tiketi ya chama cha DP

Tom Mathinji

Bunge lapendekeza kuchunguzwa kwa mfumo wa ununuzi wa KEMSA

Tom Mathinji

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi