Musalia Mudavadi: Rais Kenyatta hanipigii debe kuwa mridhi wake

Kiongozi wa Chama cha Amani Nationa Congress -ANC Musalia Mudavadi amekanusha madai kwamba anapigiwa upatu na baadhi ya viongozi wanaoegemea upande wa Rais Uhuru Kenyatta kama mridhi wake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Also Read
Rais Kenyatta amwomboleza jaji mstaafu marehemu Evans Gicheru

Mudavadi amesema atatafuta idhini ya wakenya kuwaongoza na azma yake ya kugombea urais mwaka 2022 hautegemei kuidhinishwa kwake na yeyote.

Mudavadi amesema ananuia kubadili maisha ya wakenya na kuimarisha uchumi wa nchi hii.

Also Read
Muungano wa upinzani wa NASA wasambaratika

Kiongozi huyo wa ANC amesema atazingatia zaidi uimarishaji uchumi wa nchi hii, kubuni nafasi zaidi za kazi na kuiunganisha nchi hii.

Mudavadi ambaye alikuwa akiongea Kivagala, Maragoli kaskazini katika kaunti ya Vihiga wakati wa mazishi ya marehemu Mzee Francis Chogo, aliyekuwa meya wakati wa baraza la manispaa ya vihiga alikariri haja ya wakenya kuwachunguza viongozi wanaotaka kuwachagua kabla ya kuwapigia kura.

  

Latest posts

EACC kutwaa Mali ya shilingi Milioni 216 ya afisa mmoja wa kampuni ya KETRACO

Tom Mathinji

Gavana Waiguru awaalika Wawekezaji katika Kaunti ya Kirinyaga

Tom Mathinji

Maafisa wa Utawala waonywa dhidi ya kujihusisha na siasa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi