Mutahi Kagwe: Chanjo zote zinazotolewa hospitalini ni muhimu

Huku taifa hili linapojizatiti kuhakikisha kila mkenya anachanjwa dhidi ya virusi vya Covid-19, wakenya wamehimizwa kutopuuzilia mbali chanjo zingine ambazo zimependekezwa na wizara ya Afya.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe, siku ya Alhamisi alisema serikali imejizatiti kuboresha viwango vya hospitali za serikali kuhakikisha wakenya wote wanapokea huduma bora za afya.

Akizungumza katika mahojiano na shirika la utangazaji hapa nchini KBC, Waziri huyo alisema licha ya kuwa serikali inajizatiti kuimarisha mpango wa huduma nafuu za afya kwa wote, mengi yanahitaji kutekelezwa kuhakikisha ufanisi wa mpango huo ambao ni miongoni mwa ajenda nne kuu za serikali ya Uhuru Kenyatta.

Also Read
Kenya yapiga hatua katika utoaji wa mbinu bora za upangaji uzazi

“Hatujaafikia ufanisi katika kuafikia huduma za afya wote, lakini tunaendelea juhudi. Tumefungua hospitali nyingi,” alisema Kagwe.

Also Read
Aliyekuwa Mama Taifa wa Malawi Ann Muluzi amefariki

Kagwe hakusita kutaja zimwi la ufisadi ambalo limeghubuka wizara ya Afya, ambalo alisema linadumaza uafikiaji wa malengo ya wizara hiyo.

Ili kukabiliana na ufisadi katika wizara hiyo ya Afya, Kagwe alisema ni sharti takriban wafanyikazi 100 wafurushwe kutoka makao makuu ya Wizara hiyo.

Also Read
Waziri wa zamani Joseph Nyaga ameaga dunia

“Jambo la kwanza la kukabiliana na ufisadi ni kuwaondoa wafanyikazi 100 katika jumba la afya. Kandarasi ya baadhi yao imekamilika lakini wangali wanahudumu,” alifoka Waziri Kagwe.

Seneta huyo wa zamani wa kaunti ya Nyeri, aliwarai viongozi kuiga mfano bora wa Rais mstaafu hayati Mwai Kibaki, wa kuwahudimia wakenya kwa bidii za mchwa.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi