Mutahi Kagwe: Wahudumu wa afya wafeli katika somo la Kingereza

Juhudi za Kenya za kuwatafutia ajira wahudumu wa afya nchini Uingereza, huenda zikagonga mwamba baada ya Serikali kutangaza matokeo mabaya kwenye somo la kiingereza miongoni mwa wahudumu wa afya wanaotaka kuhudumu nchini Uingereza.

Akizungumza katika kongamano la chama cha maafisa wa utabibu jijini Mombasa, waziri wa afya Mutahi Kagwe alisema kati ya wahudumu wa afya 300 waliofanyiwa majaribio ya lugha ya kiingereza, ni 10 pekee ndio waliofaulu.

Also Read
Watu 277 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Kagwe amesema matokeo hayo ni ya kutamausha, ikilinganishwa kwamba idadi kubwa zaidi ya wahudumu wa afya walioorodheshwa kwenda kuhudumu nchini Uingereza walianguka mtihani huo wa kiingereza ambao ulikuwa ni wa lazima.

Also Read
Kenya yanakili visa 144 vya maambukizi ya korona kutokana na sampuli 2,917

hata hivyo, waziri huyo alidokeza kuwa  kuna mazungumzo yanayoendelea kuhakikisha kwamba wahudumu wa afya kutoka humu nchini, wanaajiriwa katika eneo la mashariki ya kati na bara Uropa.

Waziri alisema kuwa mtaala wa utabibu utaimarishwa zaidi ili kujumuisha teknolojia ya habari, kwa kuwa taasisi za afya hapa nchini, hazitatumia mfumo wa makaratasi katika utoaji wa huduma.

Also Read
Betsafe yazindua tuzo ya mchezaji bora kila mwezi kwa timu za AFC Leopards na Gor Mahia

Maafisa hao wa kliniki pia walitaka kujumuishwa kwa mpango huo wa kutafuta kazi ughaibuni sawia na wenzao.

  

Latest posts

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

Kampuni ya sukari ya Nzoia yalaumiwa kwa kutowalipa wakulima

Tom Mathinji

China kupiga jeki uwezo wa kuzalisha chanjo hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi