Muturi awataka wanataaluma kusaidia jamii kuboresha Maisha

Spika wa bunge la taifa Justin Muturi ametoa wito kwa wana-taaluma huko Embu kufanya kila juhudi kusaidia jamii kama njia ya kuboresha maisha ya watu ambao hawajabahatika katika jamii.

Muturi ambaye alikuwa akiongea katika chuo kikuu cha Embu wakati wa kikao cha kufahamikiana na wanachama wa chama cha Embu County Professionals Development Association, alisema kuwa wanataaluma wana nafasi bora ya kuwakuza na kuwa vielelezo kwa vizazi vijavyo.

Also Read
Sifuna: ODM haina lengo la kuvuruga shughuli za uteuzi
Also Read
Bunge la kitaifa lavunja kikao cha Jumatano asubuhi kuhudhuria 'Kamukunji ya Spika'

Muturi aliwapa changamoto ya kutouliza wanachoweza kupata kutoka kwa jamii bali kuwa tayari kutoa usaidizi kwa jamii.

Aliwapa changamoto ya kuwahimiza viongozi chipukizi na wana-taaluma wanaochipuka katika jamii ili kuboresha uongozi wa siku zijazo.

Also Read
Serikali yajipanga kukabiliana na wimbi la pili la uvamizi wa nzige

Muturi alitoa changamoto kwa wanawake kutosubiri kupewa nyadhifa kubwa au kuteuliwa bungeni bali wajitokeze waziwazi kuwania nyadhifa kuu za kisiasa.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi