Muturi: Sibanduki katika kinyang’anyiro cha kuwania Urais

Mwaniaji urais wa chama cha Democratic,DP  ambaye pia ni spika wa bunge la taifa  Justin Muturi, amesisitiza kuwa atawania Urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuandaliwa tarehe tisa mwezi Agosti mwaka huu.  

Akiongea katika kanisa la  St Paul ACK mjini Sagana, Muturi alisema kuwa uvumi unaosabambazwa kuwa atajiunga na aidha muungano wa  Azimio la Umoja au ule wa Kenya  Kwanza ni wa kupotosha.

Also Read
Kenya na Barbados zaazimia kuboresha uchukuzi kati yazo

Muturi alisema “Mtakapoangalia karatasi za kupiga kura, jina langu litakuwepo,”.

Aliwaomba waumini hao kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi ili kutekeleza haki zao za kidemokrasia.

Also Read
Magavana wateule kuapishwa tarehe 25 mwezi Agosti

Aliwataka kufanya maamuzi ya busara na kuwachagua viongozi wafaao katika nyadhifa mbalimbali za uchaguzi.

Muturi pia alitoa wito kwa wawaniaji wa nyadhifa mbalimbali ambao wanataka kujiunga na chama cha  Democratic Party, kutuma maombi mapema kabla ya kufungwa kwa muda wa shughuli ya uteuzi.

Also Read
Serikali yahakikisha itakabiliana na changamoto za kiusalama wakati huu wa msimu wa Uchaguzi Mkuu

Wiki iliyopita katika eneo la  Marimanti kaunti ya Tharaka Nithi Muturi alisema kuwa alikuwa tayari kufanya mazungumzo na miungano mingine ya kisiasa.

  

Latest posts

EACC kutwaa Mali ya shilingi Milioni 216 ya afisa mmoja wa kampuni ya KETRACO

Tom Mathinji

Gavana Waiguru awaalika Wawekezaji katika Kaunti ya Kirinyaga

Tom Mathinji

Maafisa wa Utawala waonywa dhidi ya kujihusisha na siasa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi