Muyoti atwaa mikoba ya kuinoa Wazito FC

Nicholas Muyoti ameteuliwa kuwa kocha mpya wa kilabu cha  Wazito Fc kinachoshiriki ligi kuu ya soka humu nchini.

Hadi uteuzi wake Muyoti amekuwa kocha wa Kakamega Homeboyz alikosajili matokeo mazuri huku akiwa na imani kuendeleza matokeo  hayo katika timu ya  Wazito Fc.

Also Read
Kalekwa aitaka serikali kuruhusu kuanza kwa ligi kuu ya FKF

Katika majukumu yake ya ukufunzi Muyoti atasaidiwa na aliyekuwa kocha wa Muhoroni Youth  Jeff Odongo huku kipa mstaafu Mathews Ottomax akiwa mkufunzi wa makipa  .

Also Read
Wazito Fc yawafurusha wakufunzi wote siku 10 kabla ya kuanza kwa ligi kuu
Baadhi    ya       wachezaji        wa         Wazito Fc

Muyoti anachukua jukumu la kuwanoa Wazito Fc kutoka kwa Fred Ambani ambaye alitimuliwa Jumatatu pamoja na wasaidizi wake wote akiwemo msaidizi wake Salim Babu na mkufunzi wa makipa Elias Otieno.

Also Read
Uhispania wahaha kabla ya kuibandua uswizi na kutinga nuse fainali ya Euro

Timu hiyo ya Wazito ambayo zamani ilikuwa ya chuo kikuu cha Nairobi imekuwa na hulka ya kuwapiga kalamu makocha na wachezaji mara kwa mara na halieweki chanzo cha kufurushwa kwa  Ambani na wasaidizi wake.

  

Latest posts

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

FKF yakatiza mkataba wa shilingi milioni 127 na Odibets

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi