Mvua kubwa yawahofisha wakazi wa Pokot Magharibi

Wakazi wa maeneo ambayo hukumbwa na maporomoko ya ardhi na mafuriko katika kaunti ya Pokot Magharibi wameanza kuhamia maeneo salama kwa kuhofia maisha yao baada ya mvua kubwa kunyesha katika sehemu hiyo.

Hii ni baada ya matukio ya mwaka 2019 na 2020 katika kaunti hiyo ambapo mafuriko na maporomoko ya ardhi yalisababisha vifo vya watu 60.

Also Read
Mafuriko yasababisha maafa na uharibifu wa miundomsingi Nairobi

Sehemu kadhaa za kaunti ndogo ya Pokot kusini siku ya alhamisi zilishuhudia maporomoko madogo ya ardhi baada ya mvua kubwa kunyesha katika eneo hilo kwa saa kadhaa.

Naibu wa kamishna wa kaunti anayesimamia eneo la Pokot kusini, Fredrick Kimanga alithibitisha kwamba maporomoko hayo yalitokea katika kijiji cha Imonpoghet huko Lelan ingawa hakuna majeruhi walioripotiwa.

Also Read
Wahudumu wa bodaboda waonywa dhidi ya ukiukaji wa sheria

“Ningependa kuwahimiza wakazi kuhamia maeneo salama. Hawapaswi kusubiri hadi watakapokumbwa na janga,” alisema mtawala huyo.

Wakati huo huo mvua kubwa ilishuhudiwa katika eneo la Konyao na viunga vyake katika kaunti ndogo ya Pokot Magharibi na kusababisha kufurika kwa mito miwili ya Konyao na Kanyangareng.

Mwakilishi wadi ya Kapchok Peter Lorok alisema mifugo, mimea na miundo msingi imeathiriwa huku sehemu ya barabara inayovuka mito hiyo ikiwa haipitiki.

Also Read
Kaunti za Busia na Pokot Magharibi zapitisha mswada wa BBI

“Mimea yote iliyokuwa imekuzwa kando ya mito hiyo imesombwa na mafuriko hayo huku wakazi wa eneo hilo wakiwakodolea macho na ukosefu wa chakula pamoja na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu,” alisema Lorok.

  

Latest posts

Idadi ndogo ya wakazi wa Nairobi wajitokeza kuchanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 200,000 za Sinopharm kutoka China

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi