Mvutano kati ya Rosy Meurer na Tonto Dike

Kwa muda sasa kumekuwa na mvutano kwenye mitandao ya kijamii hasa nchini Nigeria ambao unahusisha waigizaji wa filamu za Nollywood Tonto Dike na Roseline Meurer.

Rosy alijipata pabaya pale ambapo alilaumiwa kwa kusababisha utengano wa Tonto Dike na Churchill Olakunle na baadaye kuolewa na Bwana Churchill huku wengi wakidhania kwamba Rose na Tonto walikuwa marafiki wa dhati.

Bi. Rosy anasema kwamba alimfahamu Olakunle ambaye ni mfanyibiashara hata kabla yake kuoa Tonto Dike na alikuwa rafiki yake na rafiki wa familia yake ambaye angewahudumia yeye, watu wa familia yake na hata marafiki na walifanya kazi pamoja.

Also Read
Stephanie Okereke Linus ateuliwa balozi wa usafi wa mazingira Nigeria.

Kulingana naye, Churchill alikuwa kama ndugu ila hawana uhusiano wowote wa ukoo na ndio maana baada ya ndoa yake na Tonto kusambaratika, mapenzi yaliota na wakamalizia kuoana.

Rosy anasema hajawahi kuwa rafiki wa dhati wa yeyote kati ya wapenzi wa zamani wa Olakunle isipokuwa alifahamishwa kuhusu Tonto kama mke wa Tonto.

Also Read
Cardi B amsifia binti ya Lebron James

Mambo yalichacha mitandaoni pale ambapo Rosy aliamua kumtakia kila la hero mtoto wa Olakunle na Tonto Dike ambaye alitimiza umri wa miaka 5 kwa jina “King”. Wengi walichukulia kitendo hicho kuwa cha unafiki kwa sababu ameonyeshwa na dhulma dhidi yake kuwa mtu aliyempokonya rafiki yake mume na hivyo kumpokonya mtoto huyo baba.

Also Read
Ni ujauzito, Chacha Eke Faani

Rose anasema naye alifahamu shutma zote dhidi yake kupitia mitandao ya kijamii lakini amejiondolea lawama zote akisema kwa muda mrefu yeye na Churchill walikuwa marafiki na uhusiano wa kimapenzi ulianza baada ya Tonto na Churchill kutengana.

Ndoa ya Tonto Dike na Churchill Olakunle ilidumu kati ya mwaka 2015 na mwaka 2017 na ndoa ya Rose Meurer na Churchill imekuwepo kwa muda wa miaka miwili sasa.

  

Latest posts

Tume Ya Filamu Yashauriana Na Wanaounda Vipindi Mitandaoni

Marion Bosire

Yul Edochie Amsifu Babake

Marion Bosire

Aki Na Paw Paw Warejea

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi