Mwamuzi wa Kenya Kamaku kusimamia mechi ya Nigeria dhidi ya Sierra Leone

Mwamuzi wa Kenya  Dkt  Peter Kamaku  ameteuliwa kusimamia mechi ya kufuzu kwa kombe la Afcon baina ya miamba wa Afrika Super Eagles ya Nigeria  dhidi ya Sierra Leone Novemba 13.

The Super Eagles watawaalika Lone Stars tarehe 13 mwezi ujao katika uwanja wa Samuel Ogbemudia huko  Benin  City kusini mwa Nigeria.

Also Read
FKF yaiomba serikali kupiga jeki Gor Mahia kwa mashindano ya kombe la shirikisho Afrika

Dkt Kamaku ambaye ni Profesa wa Hisabati katika chuo  kikuu cha  kikuu cha  Teknologia na Kilimo  cha Jomo Kenyatta  (JKUAT) atakuwa mwamuzi wa kati ikiwa mara ya kwanza kwake kualikwa kusimia mchuano wa Super Eagles.

Also Read
Mnyama Simba apaa kwenda Afrika kusini kuivaa Amakhosi

Refa huyo aliye na umri wa miaka 38 atasaidiwa na wakenya wenza Gilbert Kipkoech Cheruiyot na  Tony Mudanyi Kidiya  huku  Anthony Juma Ogwayo akiwa fourth official.

Kamaku ni miongoni mwa waamuzi 27 waliochaguliwa na shirikisho la soka barani Afrika kusimamia mechi za Afcon mwaka jana nchini Misri .

Also Read
Olunga abusu nyavu mara mbili na kuitunuku Kashiwa pointi 3

Nigeria wanaongoza kundi  L kwa pointi 6 kutokana na mechi mbili na watachuana na Sierra Leone Novemba 13 ,kabla ya kusafiri kwenda Free town kwa mechi ya marudioa .

  

Latest posts

Shujaa kuwinda pointi zaidi Edmonton 7’s

Dismas Otuke

Police Fc washerehekea kurejea ligi kuu baada ya mwongo mmoja kwa dhifa

Dismas Otuke

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi