Mwanabiashara maarufu wa Eldoret Jackson Kibor amefariki

Mwanabiashara mkongwe wa Uasin Gishu, mkulima na aliyekuwa mwanasiasa Mzee Jackson Kibor amefariki.

Kulingana na familia yake, Kibor alifariki Jumatano usiku katika hospitali ya St. Luke’s Orthopaedic and Trauma mjini Eldoret baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa familia yake, Mzee Kibor pia aliambukizwa ugonjwa wa COVID-19, na kumlazimisha kutegemea mitambo ya kumsaidia kupumua.

Also Read
Waziri Amina abanduliwa kwenye kinyang’anyiro cha Mkurugenzi wa WTO

“Kibor amekuwa akipokea hewa ya oxygen tangu mwezi Oktoba mwaka 2020 baada ya kuugua Covid-19. Alikuwa na mtungi wa gesi nyumbani na nyingine kwenye gari lake akilitumia alipokuwa akienda mjini Eldoret kutafuta matibabu,” ilisema familia yake.

Also Read
Kenya yanakili visa 1,018 vipya vya Covid-19

Hivi majuzi alikuwa amelazwa hospitalini ambako madaktari walidhibitusha kuwa Figo zake mbili ziliacha kufanya kazi.

Baadaye alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ambapo madaktari walitangaza kufakiri kwake siku ya Jumatano.

Kibor alifahamika sana kwa moyo wake wa kupeana na pia kwa hekima yake. Hata hivyo aligonga vichwa vya habari kutokana na kesi ya talaka.

Also Read
Rais Kenyatta apokea dozi ya kupiga Jeki chanjo dhidi ya Covid-19

Kibor aliyefariki akiwa na umri wa miaka 89, amewaacha wake wanne, na watoto 26 wakiwemo wakiume 16. mmoja wa wake zake alifariki.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi