Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Mwanafunzi mmoja katika shule ya upili ya Magenka iliyoko Magumoni katika kaunti ya Tharaka Nithi, aliteketeza bweni kutokana na kile kimetajwa kuwa njia ya kukwepa kufanya mitihani iliyoanza siku ya Alhamisi.

Kupitia kamera fiche za CCTV zilizoko katika afisi ya mwalimu Mkuu wa shule hiyo, mwanafunzi huyo anaonekana akiondoka darasani akielekea kwenye bweni na kisha kuuteketeza.

Also Read
Marekani yaahidi kuunga mkono juhudi za kenya za kudumisha amani

Katika kamera hizo, mwanafunzi huyo anaonekana akitoa kiberiti na kuwasha moto  godoro ambazo zilisambaza moto katika bweni nzima.

Mvulana huyo kisha alirejea darasani na kuketi kana kwamba hajatenda jambo lolote, huku akioekana kushtuka wakati habari za kutokea kwa moto zilipoenea.

Also Read
Justin Muturi: EACC ilijaribu kuhujumu safari yangu ya Ikulu

Baada ya uchunguzi, maafisa wa polisi walibaini kuwa mwanafunzi huyo hakuwa amejiandaa vilivyo kufanya mitihani hatua iliyomsababisha kuteketeza bweni hilo ili aepuke kufanya mitihani hiyo.

Matumaini ya mwanafunzi huyo ni kwamba shule hiyo ingefungwa na wanafunzi wote waagizwe kuelekea nyumbani.

Also Read
Mitihani ya majaribio kwa darasa la nane na kidato cha nne kuanza Jumatano

Hata hivyo gavana wa kaunti hiyo Muthomi Njuki alisema baada ya kukadiria hali waliazimia kuwa wanafunzi wasalie shuleni.

“Wanafunzi watasalia shuleni na kuendelea na mitihani ya,” alisema gavana huyo.
Mwanafunzi huyo alikamatwa na anazuiliwa chini ya sheria za watoto.

  

Latest posts

Idara ya Mahakama yashutumiwa kwa kuhujumu shughuli muhimu za serikali

Tom Mathinji

Uhuru Kenyatta: Usalama wa taifa hili ni shwari

Tom Mathinji

Hospitali ya Kijeshi yazinduliwa katika kambi ya kijeshi ya Kahawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi