Mwanafunzi wa kidato cha tatu akamatwa kwa mauaji ya kijusi

Maafisa wa polisi wamemtia nguvuni mwanafunzi wa kidato cha tatu baada ya kushukiwa katika kisa cha mauaji ya kijusi katika kaunti ya Kitui.

Kulingana na mwalimu mkuu wa shule, mwanafunzi huyo aliye na umri wa miaka 17 alilalamika kuhusu maumivu ya tumbo  kabla ya kupelekwa hospitalini kwa matibabu.

Also Read
Rais Kenyatta kukutana na Maseneta wa Jubilee Jumanne

Baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu, ilibainikia kwamba mwanafunzi huyo alikuwa ametoa mimba.

“Katika kituo cha afya, mwanafunzi alichunguzwa na daktari na ikabainika kwamba msichana huyo alitoa mimba. Hata hivyo alitibiwa na kuruhusiwa kuondoka,” ilisoma taarifa ya polisi.

Also Read
Rais Joe Biden amwalika Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya White House Alhamisi

Polisi walifanya uchunguzi shuleni na kupata kijusi cha miezi minane katika uwanja wa shule anakosomea msichana huyo kilichokuwa kimefungwa kwa kipande cha nguo ndani ya choo.

“Baada ya kukitoa tulipata ni kijusi cha mtoto wa kiume kikiwa kimefungwa kwa neti ya kuzuia mbu shingoni,” iliongeza ripoti hiyo ya polisi.

Also Read
Kenya yanakili visa 834 vipya vya Covid-19

Mwanafunzi huyo kwa sasa anazuiliwa na polisi huku kujusi kikipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti kwa uchunguzi zaidi.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi