Mwanahabari wa Al Jazeera auawa katika ukingo wa Magharibi

Mwana-habari wa shirika la Al Jazeera Shereen Abu Akleh, aliuawa kwa kupigwa risasi akiandaa taarifa kuhusu shambulizi la Israel katika mji wa Jenin ulioko ukingo wa Magharibi ya mto Jordan.

Also Read
Iran yataka Umoja wa Mataifa kulaani mauaji ya Mohsen Fakhri-Zadeh

Shirika hilo la habari lenye makao yake nchini Qatar lilisema kuwa Abu Akleh wa umri wa miaka 51, alipigwa risasi maksudi na kinyama na wanajeshi wa Israel.

Mwana-habari mwingine pia alijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.

Also Read
Mwanaume apachikwa moyo wa nguruwe nchini Marekani

Hata hivyo Jeshi la Israel lilikanusha kwamba vikosi vyake viliwalenga wanahabari.

Jeshi lilisema kuwa huenda walipigwa risasi na wapiganaji wa kipalestina wakati wa makabiliano ya risasi.

Also Read
Dozi ya tatu dhidi ya COVID-19 Israel yaonyesha ufanisi

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Israel Yair Lapid alikitaja kifo cha Abu Aqleh kuwa cha kuhuzunisha.

Lapid alisema watatekeleza uchunguzi kwa pamoja na halmashauri ya kipalestina kubainisha waliotekeleza shambulizi hilo.

  

Latest posts

Watu 30 watekwa nyara nchini Nigeria

Tom Mathinji

Biashara ya bidhaa za Afrika kwa njia ya mtandao wa Internet kupanua mauzo ya bidhaa za Afrika nchini China

Tom Mathinji

Ushirikiano kati ya China na Afrika unawasaidia watu wa Afrika kukabiliana na changamoto zao za kimaisha

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi