Mwanamume ashtakiwa Chuka kwa kumuua mkewe wa miaka 19

Mwanamume mmoja kutoka eneo la Igambang’ombe, Kaunti ya Tharaka Nithi, amefikishwa katika Mahakama ya Chuka kwa madai ya kumuua mkewe.

Mshtakiwa huyo, Aron Mawira Kienge, anadaiwa kumdunga kisu shingoni mkewe hadi kumtoa uhai mnamo siku ya Jumapili kutokana na sababu ambazo hazijabainika.

Kwa mujibu wa majirani wake, Mawira alikuwa na tabia ya kumpiga mkewe mara kwa mara kwa sababu zisizokuwa na msingi.

Also Read
Cyrus Oguna: Serikali yajizatiti kuangamiza nzige hapa nchini

Hata hivyo wakati wa kisa hicho, Mawira hakuwadhuru watoto wao.

Maafisa wa polisi walipofika katika eneo la tukio, walimpata mwathiriwa akitoka damu kwa wingi. Walimkimbiza hospitalini ambako baadaye aliaga dunia.

Also Read
Maafisa wa DCI wamwokoa mwanaume aliyetekwa nyara Mombasa

Mwili wake ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Chuka, huku ukisubiri kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Mshukiwa wa mauaji hayo atasalia korokoroni kwa siku 14 kwa vile anaweza kutoroka endapo ataachiliwa na pia kwa ajili ya usalama wake mwenyewe.

Also Read
Joho, Kingi, walaumiwa kwa kuhujumu usajili wa chama kipya cha Pwani

Afisa wa upelelezi wa Meru Kusini, Kennedy Kipkorir, amesema ni muhimu Mawira aendelee kuzuiliwa ili kuruhusu uchunguzi zaidi na pia kusubiri matokeo ya uchunguzi wa maiti ya mkewe.

Kesi hiyo itatajwa mnamo tarehe mbili mwezi Agosti mwaka wa 2021.

  

Latest posts

Chissano atoa wito wa mazungumzo kati ya serikali na wapiganaji

Tom Mathinji

Vifo vya ndugu wawili vyazua taharuki Embu Kaskazini

Tom Mathinji

Gladys Erude ameaga dunia

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi