Mwanamume auawa na ndovu Mtito Andei

Mwanamume mwenye umri wa miaka 73 amefariki papo hapo baada ya kukanyagwa na ndovu katika eneo la Nthunguni katika Kata ya Mtito Andei, Kaunti Ndogo ya Kibwezi Mashariki.

Muathiriwa huyo aliyetambuliwa kama Charles Mutinda Mutisya ameuawa na ndovu huyo alipokuwa akielekea shambani kwake kulima.

Also Read
Chanjo milioni moja dhidi ya korona kuwasili Kenya leo

Ndovu huyo alikuwa ametoka katika Mbuga ya Kitaifa ya wanyama pori ya Tsavo Mashariki.

Akiongea na Shirika la Habari nchini, KBC, kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi katika Kaunti ya Makueni Joseph Ole Naipeyan amethibitisha kisa hicho.

Also Read
Pembe za ndovu za thamani ya shilingi milioni 1.4 zapatikana kaunti ya Kajiado

Naipeyan amesema maafisa wa polisi kutoka Kituo cha Polisi cha Mtito Andei na Shirika la Huduma kwa wanyama pori (KWS) wamezuru eneo la kisa hicho na kupata mwili wa muathiriwa ukiwa na majeraha.

Also Read
Watalii kuingia Mbuga ya Kitaifa ya Ziwa Nakuru kupitia viingilio vya Lanet na Nderit

Mwili huo umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Makindu kufanyiwa uchunguzi wa upasuaji wa maiti.

  

Latest posts

Uhaba wa maji wakumba kaunti ndogo ya Lagdera baada ya kukauka kwa vidimbwi

Tom Mathinji

Magoha: Serikali haitabatilisha agizo lake kuhusu utumiaji wa mabasi ya shule.

Tom Mathinji

Kenya yapokea zaidi ya dozi 400,000 za chanjo ya Astrazeneca kutoka Uingereza

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi