Mwanamuziki Konshens kuwasili hapa nchini kwa tamasha la kukaribisha mwaka mpya

Mwanamuziki wa nyimbo za Dancehall Garfield Spence almaarufu Konshens kutoka Jamaica, anatarajiwa nchini Kenya Jumatano usiku tayari kwa tamasha la mwaka mpya la kukata na shoka linalosubiriwa kwa hamu na ghamu.

Wanamuziki wa hapa nchini pia hawataachwa nyuma katika kuwatumbuiza wakenya wakati wa tamasha hilo la kukaribisha mwaka mpya litakaloandaliwa katika mkahawa wa Canivore tarehe 31 Disemba.  Wanamuziki hao wa Kenya ni pamoja na Sauti Sol, Fena, Benzema na Khaligraph.

Also Read
Burna boy ashukuru wote alioshirikiana nao
Also Read
Ujio mpya wa Darubini michezo

Konshens maarufu kwa nyimbo zao Brun koff na Do Sum’n, awali wameandaa tamasha kadhaa za muziki hapa nchini, huku wakijizatiti kukutana na mashabiki wao wa humu nchini.

Also Read
Sol Family Kuandaa Tamasha Mwezi Ujao

Mwanamuziki huyo amekuwa akizungumza na mashabiki wake kupitia mitandao ya kijamii akiwahakikishia tamasha la kupigiwa mfano katika mkahawa wa Canivore.

Mara ya mwisho mwimbaji Konshens kuwa hapa nchini ilikuwa mwezi Septemba mwaka 2019.

  

Latest posts

Riadha Kenya kuandaa seminaa kwa wanariadha Januari 21 kutangulia mashindano ya kitaifa

Dismas Otuke

Brown Mauzo Azindua Video ya Kibao “Naoa”

Marion Bosire

Wadau wa Filamu Wahimizwa Kutoa Mawasilisho ya Warsha ya Durban

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi