Mwanamuziki wa Rhumba General Defao ameaga dunia

Mwanamuziki wa nyimbo za Rhumba Lulendo Matumona, almaarufu General Defao amefariki dunia Jijini Douala nchini Cameroon akiwa na umri wa miaka 62.

General Defao aliyefariki siku ya Jumatatu, alitarajiwa kuandaa tamasha la muziki kabla ya kifo chake.

Huku ikithibitisha kifo chake, Familia ya mwanamuziki huyo ilisema afya yake ilikuwa imeanza kudhoofika, huku chanzo cha kifo chake kikisalia kitendawili.

Also Read
Mtoto Noman apata kazi ya ubalozi

Familia yake ilisema saa kadhaa kabla ya tamasha hilo la muziki, gwiji huyo wa Rhumba alianza kuonyesha dalili za kuugua chumbani mwake na kisha akapelekwa katika hospitali ya Laquintinie Jijini Douala alikofariki Jumatatu Jioni.

General Defao ambaye nyimbo zake zilivuma sana katika miaka ya tisini, aliondoka nchini mwake na kuja nchini Kenya mapema miaka ya 2000, ambapo wengi walisema alitoroka kwa sababu za kisiasa.

Also Read
Kenya yanakili visa 1,018 vipya vya Covid-19

Baada ya miaka 15 nchini Kenya, Defao alirejea nchini mwake katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo tarehe nne mwezi Agosti mwaka 2019.

Also Read
Moroko wafuzu fainali ya CHAN baada ya kuwadhalilisha wenyeji Cameroon mbele ya umma

Aliporejea nchini mwake, Defao alizuru makaburi ya wanamuziki wenzake Papa Wemba, Tabu Ley, King Kester Emeneya, Madilu System na Pépé Kalle.

Punde tu baada ya kutangazwa kwa kifo chake, wanamuziki kadhaa wakiwemo Fally Ipupa, Barbara Kanam na Ferre Gola waliomboleza kifo cha mwanamuziki huyo tajika.

  

Latest posts

Riadha Kenya kuandaa seminaa kwa wanariadha Januari 21 kutangulia mashindano ya kitaifa

Dismas Otuke

Brown Mauzo Azindua Video ya Kibao “Naoa”

Marion Bosire

Wadau wa Filamu Wahimizwa Kutoa Mawasilisho ya Warsha ya Durban

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi