Mwanamuziki Waziri Ally ameaga dunia

Taifa la Tanzania linaomboleza kifo cha mwanamuziki Waziri Ally Seif mwanzilishi na kiongozi wa bendi ya Kilimanjaro maarufu kama Wana Njenje.

Jina Njenje linatokana na wimbo mmoja wa bendi hiyo ya Kilimanjaro.

Ally alikata roho usiku wa Ijumaa tarehe 23 mwezi Julai mwaka huu wa 2021 akipokea matibabu katika hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es Salaam.

Also Read
Wasanii wapata Fursa kwenye maonyesho ya SabaSaba

Wanamuziki wa Tanzania wamehuzunishwa na kifo cha mwenzao na wengi wamemwomboleza kupitia mitandao ya kijamii.

Zuhura Othman maarufu kama Zuchu, amemkumbuka mzee Waziri Ally wakati yeye na wenzake walimzuru ili kumjuza kuhusu kibao chake kwa jina “Sukari” hata kabla ya kukitoa kwa umma.

Also Read
Masharti ya Simba!

Amechapisha video fupi akiwa anasema na mzee huyo akimweleza kwamba ametumia maneno ya wimbo wa bendi yake ambayo ni “Baba Chanja” kwenye wimbo wake.

Mbosso ambaye pia ni mwanamuziki wa WCB Wasafi kama Zuchu, amemwomboleza Njenje akisema waliimba wimbo “Tulizana” ambao uko kwenye albamu yake ya Definition of Love na yeye, wakarekodi video na wakati anataka kuiachilia rasmi anapokea taarifa za kifo chake.

Also Read
Kesi ya Talaka kati ya Nicole na Dr. Dre

Mrisho mpoto yeye ameandika, “Tasinia imepata pigo la kuondokewa na Mkongwe wa Muziki. waziri njenje..

Hakika ni Pigo kubwa pole sana Familia nzima ya Kipenzi chetu. waziri.njenje”.

  

Latest posts

Kenya yanakili visa 113 vipya vya COVID-19

Tom Mathinji

Watu watano wana kesi ya kujibu dhidi ya mauaji ya wakili Willie Kimani

Tom Mathinji

Gurdian Angel Asifia Mpenzi Wake

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi