Mwanasheria mashuhuri Nzamba Kitonga kuzikwa leo

Mwanasheria mashuhuri aliyeaga dunia Philip Nzamba Kitonga anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwake katika eneo la Mutitu Wa – Ndooa, Kaunti ya Kitui.

Nzamba, ambaye amesifiwa kama mtu mashuhuri ambaye alitimiza mengi katika maisha yake, alikufa akiwa na umri wa miaka 64.

Also Read
Rais Kenyatta amwomboleza Orie Rogo Manduli

Nzamba alihudumu kama hakimu na pia mwanasheria kwa ufanisi na alikuwa mtu wa kujitolea kujenga taifa na taasisi zake.

Alikuwa mwenyekiti wa kamati ya wataalamu kuhusu marekebisho ya katiba ya mwaka wa 2010 na pia aliwahi kupigania kiti cha ugavana cha Kitui mwaka wa 2013 lakini akashindwa na Julius Malombe.

Also Read
Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Matungu Justus Murunga yasimamishwa

Ibada ya wafu ya Nzamba ilifanyika siku ya Alhamisi katika Kanisa Kuu la Katoliki la Holy Family, jijini Nairobi.

Also Read
Halfa ya uzinduzi wa ripoti ya BBI yang’oa nanga Bomas

Ameacha watoto wanne, James Ivia Kitonga, Mary Mwathi Kitonga, Kavengi Kitonga na Eve Mukami Kitonga na mjane Carol Mbuvi.

Mipango ya mazishi ya Wakili Nzamba yanaongozwa na serikali, kufuatia agizo la Rais Uhuru Kenyatta.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi