Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 48 amewaacha wakazi wa kijiji cha Rwathia eneo la Gichugu kwa mshangao baada ya kuchimba kaburi lake kabla ya kujitia kitanzi.

Kwa mujibu wa ndugu yake Elias Murimi, marehemu Joel Muthike pia aliteketeza nyumba yake moto na akasimama na panga ili kumzuia mtu yeyote kuzima moto huo.

Also Read
Kundi la waendeshaji pikipiki Meru latoa msaada wa visodo kwa wasichana

Murimi alisema kuwa baada ya marehemu kuhakikisha kuwa nyumba yake imeteketea yote alitoweka na kupatikana saa tatu baadaye akining’inia katika mti wa mwembe katika shamba la jirani.

Also Read
Mwanamke akamatwa baada ya kupatikana akiishi na maiti ya mpenziwe Eldoret

Wakazi wanasema kuwa wameripoti swala hilo kwa kituo cha polisi cha Mucagara.

Kamanda wa polisi katika eneo la Gichugu Anthony Mbogo alidhibitisha kisa hicho huku akisema kuwa polisi wameanzisha uchunguzi.

Also Read
Ada ya kuegesha magari Jijini Nairobi kutozwa kwa kila saa

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Kibugi Funeral Home ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.

  

Latest posts

Kennedy Obuya asimulia jinsi mchezo wa Ckricket ulivyobadilisha maisha yake

Dismas Otuke

Watu 19 wafariki baada ya basi kutumbukia mtoni Kaunti ya Kitui

Tom Mathinji

Watu wawili zaidi wametolewa katika migodi ya Abimbo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi