Mwanaume mmoja katika kijiji cha Kabururu katika eneo bunge la Igamba ng’ombe katika kaunti ya Tharaka Nithi anadaiwa kumuua mkewe na binti yake katika hali kutatanisha.
Jecinta Murugi mwenye umri wa miaka 27 anadaiwa kudungwa kisu na mumewe kabla ya kumkata kichwa bintiye siku ya jumamosi.
Kwa mujibu ya jamaa zake ambao waliwasili mahala hapo, wawili hao walikutana chuoni na baadaye mwanamke huyo akajifungua mtoto ambaye kwa sasa ana umri wa miaka sita.
Hata hivyo walianza kuzozana na kutengana kwa miaka kadhaa. Naibu kamishna wa kaunti katika eneo la Igamba ng’ombe Fred Masinjila alisema kuwa mwanaume huyo alienda mafichoni na msako dhidi yake umeanzishwa.
Naibu huyo wa kamishna alisema maafisa wa upelelezi wa jinai DCI wanamsaka mshukiwa huyo ambaye ametajwa kuwa hatari na aliyejihami.