Mwanaume mmoja akamatwa kwa kumnajisi na kumtunga mimba bintiye

Maafisa kutoka idara ya upelelezi wa jinai siku ya Ijumaa walimkamata mwanamme wa umri wa miaka 35 kwa madai ya kumnajisi mara kadhaa bintiye mwenye umri wa miaka 13 na kumtunga mimba.

Kisa hicho kilitokea katika sehemu ya Kagumo kaunti ya Murang’a.

Also Read
Majambazi wawili wauawa na polisi mtaani Eastleigh

Kulingana na idara ya upelelezi wa jinai DCI, mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Gatumbi alimpeleka mwanafunzi huyo wa darasa la tano hadi katika hospitali moja ya eneo hilo kwa uchunguzi baada ya kushuku kuwa alikuwa mja mzito.

Also Read
Afisa wa KDF akamatwa kwa madai ya utekaji nyara Kasarani

Hospitali hiyo ilithibitisha kuwa msichana huyo alikuwa na mimba ya miezi sita.

Idara ya DCI imesema uchunguzi uliofanywa na hospitali hiyo ulifichua kuwa babaye msichana huyo ndiye aliyemtunga mimba.

Also Read
Je, ni nani atashtakiwa katika kashfa ya Mabwawa ya Arror na Kimwarer?

Msichana huyo alielezea jinsi babake alivyomnajisi mara kadhaa tangu mwezi Julai mwaka uliopita.

Msichana huyo sasa anatunzwa na afisa wa watoto katika kituo cha uokoaji cha Muthithi, wakati mshukiwa akizuiliwa na huku uchunguzi ukiendelea.

  

Latest posts

Prof. Magoha: Mtaala mpya wa elimu hautatupiliwa mbali

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Nelson Havi awasilisha rufaa ya kusimamisha mtaala wa CBC

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi