Mwandishi wa vitabu Salman Rushdie ashambuliwa nchini Marekani

Salman Rushdie, mwana-riwaya kutoka Indian ambaye alitumia miaka mingi akiwa mafichoni baada ya Iran kutangaza zawadi kwa yeyote atakayekata kichwa chache, alidungwa kisu akiwa jukwaani hapo jana katika ukumbi moja wa taasisi ya masomo huko New York, Marekani.

Alikimbizwa hospitalini kwa ndege, kulingana na duru za polisi na baada ya upasuaji uliochukua masaa kadhaa, alikwua amewekwa kwenye vipumzi na hangeweza kuongea.

Also Read
Mchina anayejitolea Kukuza Ndoto za Watoto wa Makazi Duni Kenya

Shambulizi hilo limekashfiwa na waandishi na pia wana-siasa kote duniani, wakilitaja kuwa ukiukaji wa haki za kujieleza.

Rushdie mwenye umri wa miaka 75, alikuwa akijulishwa ki-rasmi ili kuhutubia ma-mia ya watu kuhusu uhuru wa wasanii, katika taasisi ya Chautauqua iliyoko magharibi mwa Jiji la New York, wakati mtu mmoja alipopanda haraka jukwaani na kumdunga kisu mwana-riwaya huyo, ambaye amekuwa akiishi huku kukiwa na zawadi iliyotangazwa miaka 1980 kwa yeyote atakayemkata kichwa.

Also Read
Marekani yaitaja China kuwa tishio kubwa kwa demokrasia duniani

Umati uliopigwa na butwaa ulisaidia kutenganisha mtu huyo na Rushdie, ambaye alikuwa ameanguka sakafuni.

Also Read
Tundu Lissu: Uchaguzi mkuu wa Tanzania ulikumbwa na udanyanyifu

Maafisa wa idara ya polisi ya New York ambao walikuwa wamepiga doria mahala hapo walimtua nguvuni mtu huyo.

Baadaye mshukiwa huyo alitambuliwa na polisi kuwa Hadi Matar, mwenye umri wa miaka 24 kutoka Fairview, jimbo la New Jersey, na ambaye alikuwa amejikatia tiketi ya kuhudhuria hafla hiyo.

  

Latest posts

Boro wamtimua meneja Chris Wilder kwa matokeo duni

Dismas Otuke

Marekani kutatua mzozo wa mpakani baina ya Israel na Lebanon

Tom Mathinji

Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi Burkina Faso Paul-Henri Damiba ajiuzulu

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi