Mwaniaji Urais wa Muungano wa Azimio Ahudhuria Ibada

Huku majibu ya uchaguzi wa urais yakisubiriwa kwa hamu na ghamu mwaniaji urais wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga anahudhuria ibada ya Jumapili siku kadhaa baada ya siku ya kupiga kura. Hii ndio mara ya kwanza Odinga anaonekana hadharani baada ya kupiga kura siku ya Jumanne.

Also Read
Kamati ya Kusaidia Rais Mteule Kuchukua Hatamu za Uongozi Yaanza Kazi Rasmi

Mbunge mteule wa eneo bunge la Lang’ata katika kaunti ya Nairobi Felix Odiwuor maarufu kama Jalang’o na katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini COTU Francis Atwoli wanahudhuria ibada pamoja na Odinga katika kanisa la mtakatifu Francis ACK huko Karen.

Also Read
Uchaguzi mkuu nchini Iran wavutia Idadi ndogo ya wapiga kura

Alipopata fursa ya kuzungumza kanisani, Raila alinukuu sehemu ya sala ya mtakatifu Francis wa Assisi ambayo ni;

Bwana, nifanye chombo cha amani yako;
Ambapo kuna chuki, napenda kupanda upendo;
Ambapo kuna kuumia, msamaha;
Ambapo kuna kosa, ukweli;
Ambapo kuna shaka, imani;
Ambapo kuna tamaa, tumaini;
Ambapo kuna giza, nuru;
Na ambapo kuna huzuni, furaha.

Also Read
Wakazi wa Kiambu wakadiria hasara kutokana na hitilafu za umeme zinazoteketeza nyumba zao

Huku hayo yakiendelea, shughuli ya kuhakiki fomu nambari 34A kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi katika kiwango cha maeneo bunge inaendelea katika kituo kikuu cha kitaifa cha kujumlisha kura huko Bomas of Kenya.

  

Latest posts

Wabunge wa kaunti ya Kitui wataka baa la njaa kutangazwa janga la kitaifa

Tom Mathinji

Wakazi wa Baragoi wahimizwa kuishi kwa amani

Tom Mathinji

Malkia Strikers warejea nyumbani kinyemela baada ya kubanduliwa mashindano ya dunia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi