Nabulindo amrai Mudavadi kujiunga na Raila katika Azimio la Umoja

Mbunge wa eneo bunge la Matungu ,Peter Oscar Nabulindo, amemtaka kiongozi wa chama cha Amani National Congress(ANC) Musalia Mudavadi ,kujiunga na Raila Odinga kwenye muungano wa Azimio la Umoja .

Nabulindo aliyechaguliwa mbunge wa Matungu kupitia chama cha ANC ,amesema ni wakati mwafaka na jambo la busara kwa Mudavadi kutoa mwelekeo wa chama mapema kwa kujiunga na Azimio la Umoja .

Kulingana na Nabulindo muda uliosalia kabla ya uchaguzi mkuu ni mchache mno, na itakuwa bora kwa ANC kuamua hatma yake kwa wafuasi na pia kwa wale wanaopanga kuwania viti kwa tiketi ya chama hicho.

Also Read
Serikali ya Kakamega yatakiwa kuwafidia wahudumu wa afya waliofariki kutokana na Covid-19

Nabulindo anahoji kuwa kiongozi huyo wa ANC atakuwa na fursa nzuri kuwa kwenye serikali ijayo akibuni muungano na Raila kuliko kubuni muungano na chama cha UDA.

“Namwomba kiongozi wa chama changu kutoa msimamo na mwelekeo ,mapema na kuunda muungano na Raila katika Azimio la Umoja , ili watu wajipange maana ukiangalia muda uliosalia kabla ya uchaguzi ni mfupi sana”akasema Nabulindo

Mbunge huyo pia ametangaza kumuunga mkono Raila Odinga anayewania Urais kupitia azimio la Umoja ,akiwa mbunge wa pili wa ANC kufanya hivyo ,baada mbunge wa Lugari Ayub Savula kutangaza kuunga mkono Azimio la Umoja, kwenye mkutano wa kisiasa ulioandaliwa uwanjani Bukhungu kaunti ya Kakamega tarehe 31 mwezi uliopita.

Also Read
PSG na Basaksehir kurudia mechi yao Jumatano usiku

“Sijahama ANC ,bali ni kutangaza tu msimamo wangu kwani ukiangalia huku Matungu watu wengi wanaegemea muungano wa Azimio sawa tu na vile Ayub Savula pia alifanya na pia seneta Cleo Malala ambaye alitangaza kumuunga mkono naibu Rais William Ruto ” akaongeza Nabulindo

ANC imeiitisha kikao kikuu kwa wanachama wote nchini (NDC) katika ukumbi wa KICC tarehe 23 mwezi huu ambapo inatarajiwa kuwa Mudavadi atatangaza msimamo wa chama kwenye uchaguzi wa Urasi Agosti mwaka huu.

Also Read
Morans wapakatwa na Angola michuano ya kufuzu kwa Fiba Afrobasket

Kumekuwa na tetesi na minong’ono kuhusu hatma ya Mudavadi katika harakazi zake za kugombea Urais, wengine wakidokeza kuwa huenda akabuni mungano na chama cha United democratic Alliance(UDA) kinachoongozwa na Naibu Rais William Ruto.

Mudavadi amekuwa kwenye muungano wa One Kenya Alliance (OKA) tangu mwaka uliopita huku wakisimama kidete kuwa wangali ndani ya OKA na wala hawana nia ya kugura.

Mudavadi amekuwa akishawishiwa sana na Ruto kubuni muungano na UDA ,huku kiongozi wa chama cha Wiper Stephen Kalonzo akidokezwa kuwa njiani kuunda muungano na muungano wa Azimio la Umoja chini ya uongozi wa Raila .

  

Latest posts

Shujaa kulenga kuboresha matokeo Sevilla 7’s baada ya kutepetea Malaga

Dismas Otuke

Nchi za Afrika zaunga mkono Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing

Tom Mathinji

Isaac Juma Shabiki mashuhuri wa Harambee Stars na AFC Leopards auawa kikatili Mumias kutokana na mzozo wa ardhi

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi