Nadia Mukami Atambulisha Msanii

Mwanamuziki Nadia Mukami ametambulisha msanii ambaye amemhusisha katika kibao chake cha kwanza. Msanii huyo wa kiume anafahamika kama Latinoh na kibao chake cha kwanza kinaitwa “Siwezi” na amemshirikisha Nadia. Kazi hiyo imezinduliwa hii leo kwenye mtandao wa You Tube.

Also Read
Asante kwa kutangaza imekuwa vigumu kuweka hii siri!

Awali Nadia alikuwa amemsifia mwimbaji huyo wa umri wa miaka 22 kutoka eneo la Likoni kaunti ya Mombasa. Nadia anasema alivutiwa na weledi wa kijana huyo katika kuandika nyimbo na kuimba ndipo akaamua kumsajili chini ya kampuni yake inayofahamika kama Sevens Creative Hub.

Also Read
Arrow Bwoy Aandaliwa Sherehe ya Siku ya Kuzaliwa

Latinoh ndiye msanii wa kwanza ambaye amesajiliwa chini ya mbawa za Nadia Mukami msanii ambaye amekuwa akifanya vizuri siku za hivi karibuni. Msanii huyo ambaye pia hujirejelea kama African Pop Star amekaribisha wengine ambao wana vipaji wajisajili na kampuni yake.

Also Read
Happy Birthday Nadia Mukami!

Sikiliza kibao cha Latinoh na Nadia hapa;

  

Latest posts

Kibao kipya cha Nonini kuzinduliwa siku ya kuzaliwa kwake

Tom Mathinji

Brenda Jons atangaza kuwa sasa ameokoka

Tom Mathinji

Msanii wa Marekani Coolio ameaga dunia

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi