Nafasi ya Kenya kwenda AFCON 2022 yadidimia baada ya kukabwa koo na Comoros

Timu ya taifa Harambee Stars haina budi kuishinda Comoros katika marudio  ya Jumapili hii ya  mechi ya kundi G kufuzu kwa dimba la AFCON mwaka 2022 .

Stars baada ya kulazimishwa sare nyumbani dhidi ya Comoros Jumatano usiku katika uwanja wa Kasarani sasa wanajikuta  kweny njia panda ambapo ni sharti wazoe angaa pointi moja ili kuwa na fusra vya kufuzu.

Also Read
Harambee Stars yabweteka nyumbani na kwenda sare tasa na Uganda mechi ya kufuzu kombe la dunia

Endapo Kenya itapoteza Jumapili ugenini dhidi ya Comoros basi  itakuwa rasmi kuwa nafasi yao ya kufuzu kwenda Cameroon itakuwa chini ya asilimia 10 .

Comoros wanaongoza kundi  G kwa alama 5 kufuatia mechi tatu  wakishinda pambano moja na kutoka sare mbili wakifuatwa na Kenya wenye pointi 3 baada ya kutoka sare tatu.

Also Read
Rising Stars tayari kwa mashindano ya Cecafa

Hata hivyo msimamo huo utabadilika pakubwa endapo mabingwa mara 7 wa AFCON Misri wataishinda Togo jijini Cairo Jumamosi  hii ,kwani wataongoza kundi  hilo kwa pointi 5 sawia na Comoros huku pia Togo wanaweza kuipita Kenya na kuwa na alama 4 endapo wataishinda Misri.

Also Read
Ni Siku ya Ndovu kumla mwanawe Tusker dhidi ya Zamalek Nyayo

Kenya imesalia na mechi tatu za kucheza ambapo wataanzia mjini Moroni Jumapili hii,na kisha baadae  Machi 22 mwaka ujao na kufunga ratiba kwa ziara ya Lome kumenyana na wenyeji Togo tarehe 30 mwezi Machi mwakani.

  

Latest posts

Wakenya Rotich na Tanui wavunja rekodi za Paris na Amsterderm Marathon

Dismas Otuke

Tusker waleweshwa nyumbani na Zamalek 1-0

Dismas Otuke

Tysa yasherekea miaka 20 ya kubadilisha vijana Kitale kupitia soka

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi